Saturday, July 4, 2015

NIUNGENI MKONO WANANEWALA WOTE

Namshukuru Mwenyezi Mungu muummba wa mbingu na ardhi na vilivyomo humo na vilivyo baina ya mbingu na ardhi. Ninania ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Newala Vijijini tukijaliwa kupata jimbo na kama vigezo havitakidh i vya kupata jimbo basi inshaallah nitagombea jimbo la Newala natarajia kupitia Chama cha Mapinduzi.

Ombi langu kubwa kwenu wadau wa blog hii  na WanaNewala mniunge mkono kwania yangu hii. Naingia nikiwa najua kuwa ninadhima kubwa ya kurudisha matumaini kwa wanainchi waliokosa imani kwa chama cha mapinduzi na serikali yake, vilevile najua kuwa kuna makundi hayajaguswa kabisa.

Ninania  ya dhati kabisa naomba mniunge mkono kwa hali na mali ,  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili Wananewala inshaallah. Changamoto  za Newala wala hazihitaji elimu ya chuo kikuu kuweza kuzibaini au kuzitatua bali zinahitaji umoja, mshikamano na uongozi madhubuti chini ya Fakihi Mshamu kama Mbunge mtarajiwa wa Jimbo jipya la\ Newala.

Wadau wenzangu wa Newala, kumbukeni  kuwa mageuzi ya aina yeyote yanahitaji  mambo makuu mawili; wakati  na umoja. Ni matumaini yangu kuwa wakati umekwishafika kilichobaki ni ninyi kuungana nami na kuunda umoja ili tulete mageuzi. Nakuja kwenu nikijua kuwa HAYA TULIYONAYO NDIO MAISHA YENYEWE NA HAKUNA MAISHA MENGINE ZAIDI YA HAYA TULIYONAYO KWA HAPA  DUNIANI NA KILA AHADI NI  YENYE  KUULIZWA  MBELE  YA MWENYEZI MUNGU.

Tunayo  mengi yenye tija kwa  ustawi wa Wananewala, wakati ukifika tutawaelezeni  na tutawaomba mtuunge mkono. WITO WANGU  KWENU NI KUWA MAKINI  NA  WAGOMBEA  WATAKAOJARIBU  KUZINUNUA AKILI  ZENU ILI MSIFANYE CHAGUO  SAHIHI, KUMBUKENI KUWA MIAKA MITANO NI MINGI SANA ENDAPO MTAKUWA KATIKA SHIDA  NA  M ANUNG'UNIKO  NA NI MICHACHE ENDAPO MTAKUWA KATIKA FARAJA NA FURAHA, AKILI YAKO  NDIO  DHAMANA  YAKO.

Friday, June 12, 2015

TUJIHADHARI NA WAGOMBEA WATOA RUSHWAKila sifa njema ni zake  Mwenyezi Mungu aliyemuumba Mwanadamu  katika umbo bora. Watanzania wenzangu, uchaguzi unapokaribia, wagombea huonekana wapole, wakarimu, wenye kauli zenye matumaini na wenye kuwajali wananchi. Kabla na baada ya uchaguzi ukali, majivuno, dharau na ubabe kwa wananchi huwa ndio kawaida yao.
Leo si ajabu kuwaona wagombea wakigawa fedha, nguo na vitu vingine bila hata kuombwa. Tunawapongeza kwa moyo wao wa kutoa lakini wanatakiwa watupe majibu kwa nini misaada yao ije wakati huu wa uchaguzi na si kabla ya hapo? Vitu hivi ni nini kama si RUSHWA? Watanzania wenzangu, hivi tuko tayari kuuza ukristo na uislamu wetu? Dini zetu zinatuonya juu ya kutoa na kupokea RUSHWA. Uislamu, mtume Muhammadi (S.a. w) anasema “Mwenyezimungu amemlaani mtoa Rushwa,mpokea Rushwa na anayewaunganisha wawili hawa”. Katika Qur’ani Mwenyezimungu anasema”NA UTAWAONA WENGI KATIKA WAO WANAKIMBILIA KATIKA DHAMBI NA UADUI NA ULAJI WAO WA HARAMU. BILA SHAKA WAYAFANYAYO HAYO NI MABAYA KABISA (Q 5:62)” Ndani ya Bibilia nako wakristo wamekemewa vibaya”. KWELI JEURI HUMPUMBAZA MWENYE HEKIMA, NA RUSHWA HUHARIBU UFAHAMU (MHUBIRI:7:7).
Watanzania wenzangu RUSHWA ni kipimo cha kumtambua kiongozi bora na asiyebora. Kama mgombea akikujia kukuomba kura yako na kukupa kitu kidogo ujue wazi kuwa huyo amepoteza sifa ya kuwa kiongozi, ukimchagua kiongozi kwa sababu tu ametoa RUSHWA ujue kuwa ni kumpa meno yatakayo mjengea dharau na majivuno juu yako. Akichaguliwa kwa njia ya RUSHWA kiongozi hujiona pesa zake ndizo zilizomchagua na si wewe mtanzania mwenzangu uliyempigia kura.
Leo ukitangaza nia ya kugombea nafasi fulani watu watakuuliza “unapesa?”. Tabia hii ndiyo inayopelekea tupate viongozi wabovu ati kwa sababu tu wanapesa, asiyekuwa na pesa hata kama anasifa njema  watu hawamjali. Naikumbusha nafsi yangu na yako ewe uliyejaliwa akili timamu, RUSHWA ni adui katika jamii, Serikalini na katika dini, tujilazimishe kuikataa ili tusichague PUMBA tukaacha MCHELE.
Poleni watanzania wenzangu mnaodanganyika kwa sasa mkawa tayari  kupokea RUSHWA na kujiingiza katika upofu wa maamuzi. Ombi langu kwenu mchagueni kiongozi bora na si bora kiongozi, hata kama mtu amewajieni kwa baiskeli lakini akawa na hoja thabiti zinazoonesha matumaini mchangueni atawafaeni kuliko huyo mtoa RUSHWA.
FAKIHI S. MSHAMU (MWL NAHONYO).
SIMU: 0784950236/0712829903.
Blog:www.nahonyo.blogspot.com.


MFAHAMU FAKIHI MSHAMU (MWL NAHONYO).


Huyu ni mwalimu kitaaluma. Ni mtoto wa Mzee Salumu Mshamu na Bi Esha Namalove wa Mtongwele Chilangala Wilayani Newala Mkoani Mtwara.
Alizaliwa tarehe 01/05/1980 katika kijiji cha Mtongwele  Chilangala.
1989 – 1995: Alisoma elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mbonde wilaya ya Newala.
1996 – 1999: Alisoma elimu ya sekondari katika shule ya kutwa Mnyambe Wilaya ya Newala .
2003: Alijiunga na chuo cha ualimu Bustani Wilayani Kondoa mkoani Dodoma kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti.
2004: Aliajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kama Mwalimu na alipangiwa shule ya Msingi Mbonde ambako anafundisha hadi leo.
2010: Alifanya mtihani wa kidato cha sita (6) katika shule ya Ndanda kama mwanafunzi wa kujitegemea. Baada ya matokeo alijiunga na chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ambako alihitimu na kutunukiwa shahada ya Ualimu (B.A Education) Mwaka 2013.

Friday, June 5, 2015

MFAHAMU FAKIHI SALUMU MSHAMU (MWL. NAHONYO)

Huyu ni mwalimu kitaaluma aliyefikia chuo kikuu. Huyu ni mtoto wa Mzee Salumu Mshamu na Bi Esha Namalove wa Mtongwele Chilangala wilayani Newala.
Alizaliwa tarehe 01/05/1980 katika kijiji cha Mtongwele Chilangala, mwaka 1989-  1995 alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi Mbonde wilayani Newala.
Mwaka 1996 -  1999 alisoma elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya kutwa Mnyambe wilayani Newala.
Mwaka 2003 alijiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Bustani wilayani Kondoa mkoani Dodoma kwa ngazi ya cheti.
Mwaka 2004 aliajiriwa na Halmashauri ya Wilaya kama mwalimu wa shule ya msingi Mbonde.
Mwaka 2010 alifanya mtihani wa kidato cha sita kama mtahiniwa wa kujitegemea, baada ya matokeo alijiunga na chuo kikuu cha waislam Morogoro kwa ajili ya shahada ya ualimu ambapo mwaka 2013 alihitimu na kutunukiwa shahada.

TUNU ALIYOJALIWA; NGAZI ZOTE ZA UALIMU ALIZOPITIA AMEWAHI KUWA KIONGOZI. MAASHAALLAH

Thursday, May 9, 2013

ATHARI ZA NGOMA YA N’DOMO NA BAKULI KWA UTAMADUNI WA WAMAKONDE

 ATHARI ZA NGOMA YA N’DOMO NA BAKULI KWA UTAMADUNI WA WAMAKONDE
Fakihi Salumu Mshamu
MUM/T/10/1787
Shahada ya ualimu
Bwana Hamad A.S
Ripoti Ndogo ya Utafiti kwa Masharti ya Kutunukiwa  Shahada ya Ualimu katika Kitengo cha Kiswahili,Idara ya Lugha, Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro
Machi 2013


                                                 TAMKO LA UMILIKI
(a)Tamko la Mtafiti
Ripoti hii ndogo ya utafiti inatokana na juhudi yangu mwenyewe haijawahi kuwasilishwa  mahali popote kwa dhumuni lolote,
JINA ------------------------------------------------------------- Namba ya usajili ----------------
SAHIHI --------------------------------------------------------- TAREHE -------------------------

(b)Tamko la Msimamizi
Ripoti hii ndogo ya utafiti imewasilishwa kwangu kupata ridhaa nikiwa kama msimamizi niliyeteuliwa na chuo cha waislamu Morogoro
JINA ……..                                            IDARA
SAHIHI  ___________                                   TAREHE ________________________
                                                  SHUKRANI                                                
 Napenda kuwashukuru wote walio niwezesha kufanikisha utafiti huu kwani bila wao ningekwama na kuishia njiani. Miongoni mwao ni pamoja na Bwana Abdallah Suleimani Hamadi ambaye ni mwalimu wangu aliyenipatia mwongozo kwa kila hatua ya utafiti niliyopitia. Shukrani zangu pia ni kwa wake zangu, Bi. Zakia Mkapunda na Bi. Khadija Mbarouk ambao wakati wote walikuwa wavumilivu na wasubirivu pale nilipokuwa ninashughulika na utafiti huu  walitoa mchango mkubwa kabisa katika kukamilisha kazi hii.

Nawashukuru pia wale wote walioniwezesha kupata taarifa mbalimbali ambao ni pamoja na Mwl. Ibrahim Jumanne (MEK), Mohamedi Jumanne (M/TJ), Mzee Ahmadi Twalibu (Mpiga ngoma), Hawa Nambung’o (Mcheza ngoma )Mariamu Khamisi (mcheza ngoma) na Amiri Chimbanga wote hawa ni kutoka kata ya Chihangu.

Shukrani za pekee ni kwa Bi.Anzilani Saidi kwa kufanya kazi ya kuchapa ripoti hii. Niseme tu  kuwa, nawashukuru wote walioniwezesha kufanikisha kazi hii. Hata kama jina lako sijalitaja ufahamu kuwa mchango wako ninauthamini na ninamuomba Mwenyezi Mungu awajalie wote mafanikio hapa duniani na kesho Akhera.                                                       TABARUKU
Tabaruku za kazi hii ziwafikie wazazi wangu wapendwa,Mzee Salumu Mshamu na Bi Esha Namalove wote wa K.C Mtongwele II Wilayani Newala. Walezi wangu Ahmadi  Nanyalika (Mwenyezi Mungu amrehemu ) na mke wake, Hawa Binti Mwalimu wote wa Mnyambe Wilayani Newala. Pia napenda kutabaruku kazi hii kwa wanangu, Shamzaki Fakihi na Milumba Fakihi pamoja na kaka na dada zangu wote.    

                                                     YALIYOMO
TAMKO LA UMILKI ------------------------------------------------------------------------------
Tamko la Mtafiti -------------------------------------------------------------------------------------
Tamko la Msimamizi -------------------------------------------------------------------------------
SHUKRANI ------------------------------------------------------------------------------------------TABARUKU--------------------------------------------------------
YALIYOMO -----------------------------------------------------------------------------------------
VIFUPISHO NA UFAFANUZI WA ISTILAHI -----------------------------------------------
ORODHA YA MAJEDWALI ---------------------------------------------------------------------
IKISIRI------------------------------------------------------------------------------------------------SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.0              Utangulizi
1.1       Usuli wa Mada
1.2       Ufafanuzi wa Mada  
1.3       Madhumuni ya Utafiti
1.3.1    Lengo la Jumla
1.3.2    Malengo Mahsusi
1.4       Umuhimu wa Utafiti
1.5       Maswali ya Utafiti
1.6       Sababu za Kuchagua Mada
1.7       Vikwazo vya Utafiti
SURA YA PILI
MAPITIO YA KAZI TANGULIZI
2.0              Utangulizi
2.1       Yaliyoandikwa kuhusu Mada
2.1.1    Yaliyoaqndikwa kuhusu Ngoma
2.1.2    Yaliyo andikwa kuhusu Wamakonde
2.1.3    Yaliyoandikwa kuhusu Utamaduni
2.2       Mapungufu ya Kazi Tangulizi
2.3       Kitu Kipya Kilichoonyeshwa na Utafiti
 SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.0              Utangulizi
3.1              Mpango wa Utafiti

3.2              Eneo la Utafiti
3.3              Walengwa wa Utafiti
3.4              Watafitiwa
3.5              Mipaka ya Utafiti                                           

3.6              Zana na Vifaa vya Utafiti
3.7              Mbinu za Ukusanyaji wa Data
3.7.1           Dodoso
3.7.2            Hojaji
3.7.3            Ugunduzi Makini
                             3.7.4       Uzoefu wa Mtafiti
3.8              Udhibiti wa Data
3.9              Mbinu za Uchanganuzi wa Data
SURA YA NNE
TAARIFA ZA UTAFITI
4.0              Utangulizi

 4.1            Uwasilishaji wa Data
4.1.1   Majibu ya Madodoso ya Vijana wenye Umri wa Miaka 15- 39                      4.1.1.1       Faida za Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.1.1.2     Madhara ya Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.1.1.3     Sababu za Vijana kutopenda Kucheza N’goma ya N’domo na Bakuli
4.1.1.4    Mambo yanayoweza Kuboresha na Kuendeleza Ngoma ya N.domo na Bakuli
4.1.2       Majibu ya Madodoso ya Wazee wenye Umri wa Miaka 40- 80
4.1.2.1    Faida za Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.1.2.2    Udhaifu wa Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.1.2.3    Nyimbo za Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.1.2.3.1   Nyimbo za ngoma ya N’domo
4.1.2.3.2   Nyimbo za Ngoma ya Bakuli
  4.1.2.4   Sababu za Vijana Kutopenda Ngoma
4.1.2.5    Mambo yanayo werza kubolesha ngoma
4.2.1    Ngoma ya N’domo
4.2.2    Ngoma ya bakuli
4.3       Mjadala
4.3.1    Ufaafu wa Ngoma ya N’domo na Bakuli kwa Utamaduni wa Wamakonde
4.3.2    Udhaifu wa Ngoma ya N’domo na Bakuli
4.3.3    Sababu za Vijana Kutopenda Ngoma
4.3.4    Mambo Yanayoweza Kuboresha Ngoma
SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.0       Utangulizi
5.1       Muhtasari
5.2       Hitimisho
5.3       Mapendekezo
MAREJEO                                                                                           VIAMBATANISHO
           

                 VIFUPISHO NA UFAFANUZI WA ISTILAHI
VIFUPISHO
Bi…………. Bibi
Mwl ………..Mwalimu
MEK ……….. Mratibu Elimu Kata
M/TJ …………. Mwenyekiti wa kijiji

UFAFANUZI WA ISTILAHI
Likuti ____ Ngoma kubwa inayotumika katika uchezaji wa ngoma ya mdomo
likungwa ____ Ngoma ndefu ambayo hutumika wakati wa kucheza ngoma ya bakuli  
Mkumi…………….. Shughuli za pamoja katika uzalishaji mali
Chama…………….. shughuli zinazofanywa kwa ushirika kwa zamu zamu
Indunda……………..Ngoma ndogo inayotumika wakati wa kucheza ngoma ya n’domo na bakuli

                  ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali namba 1:Kategoria za Watafiti
Jedwali namba 2: Makundi ya ufafanuzi  wa ngoma
Jedwali namba 3: Ufafanuzi wa ngoma
Jedwali namba 4: Sababu ya vijana kutopenda ngoma
Jedwali namba 5: Udhaifu wa ngoma ya N’domo na Bakuli
Jedwali namba 6: Mambo yanayoweza kubolesha ngoma
                                     IKISIRI
Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde ni utafiti ulioonyesha nafasi ya ngoma za asili katika kuendeleza na kudumaza maadili ya Wamakonde Wilayani  Newala. Katika kuendeleza utamaduni wa  Wamakonde ngoma inachukua nafasi kubwa sana. Pamoja na utamaduni kuwa na vipengele vingi utafiti huu umegusia kipengele cha ngoma tu ambapo mtafiti amejishughulisha na ngoma ya N’domo na Bakuli.

Kuhusu ngoma Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana (1979) wanasema, “Taifa letu lina utajiri mkubwa wa ngoma, ngoma hizi kiasi zina shabaha maalum ya kudumisha na kustawisha jamii.” Mbonde (1993) anasema “Wamakonde wanazo ngoma za namna  nyingi. Ambazo ni za kustarehesha sana.’’ Balisidya (1987) anaamini kuwa “kupitia ngoma tunaweza kupata nyimbo za kishairi zenye kutumia mahadhi, melodia, mkongoso na muala.”

Utafiti huu ulilenga kubaini uzuri na ubaya wa ngoma ya N’domo na Bakuli pamoja na kubaini sababu zinazopelekea ngoma za asili Wilayani Newala kutoweka na kukosa mvuto kwa vijana wa wilaya hiyo.
Katika ukusanyaji wa data mbinu zilizo tumika ni pamoja na uzoefu wa mtafiti, ushuhudiaji, dodoso na hojaji. Utafiti huu utawasaidia watu mbalimbali walioko shuleni na wasiokuwepo  shuleni kwani utafiti huu utawezesha watu mbalimbali kufahamu zaidi kuhusu ngoma ya n’domo na Bakuli kwa kina zaidi.

Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni watu wazima 35 na vijana 25 wakike na wakiume katika kata ya chihangu na  Mnyambe wilayani Newala.
Utafiti huu uligundua nyimbo za ngoma ya N’domo na Bakuli, mbinu zinazowezakuboresha ngoma hizi au kuendeleza ngoma za asili na sababu zinazo pelekea vijana kutopenda kushiriki katika uchezaji wa ngoma.
Katika kufanya utafiti mtafiti alikutana na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na tatizo la usafiri, kukosekana kwa marejeo ya kutosha na ushirikiano mdogo kwa watafitiwa. Mtafiti alijitahidi kadri ya uwezo wake kukabiliana na changamoto hizo kwakujaribu kuelimisha watafitiwa umuhimu wa utafiti ili kuondoa /kupunguza changamoto za utafiti zilizomkabili.

Utafiti huu umechukua muda wa miezi minne (4) November hadi Machi na kiasi cha shilingi 800,000/=kimetumika katika kukamilisha utafiti huu.    


UTANGULIZI
Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde ni mada ya utafiti huu ambayo mtafiti ameitafiti na ameweza kufanikiwa kukamilisha utafiti wake. Katika utafiti huu mtafiti alijishughulisha na vipengele mbalimbali kama vile nyimbo za ngoma ya n’domo na bakuli ufaafu na udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli, sababu zinazopelekea vijana kutopenda kushiriki katika uchezaji wa ngoma za asili hasa ngoma ya n’domo na bakuli na mambo ambayo yanaweza kuboresha au kuendeleza ngoma za asili Wilaya ya Newala.

Mtafiti amefanikiwa kutembelea Wilayani Newala na kuonana na Wamakonde ambao ndio wahusika  na uchezaji wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa kiasi kikubwa mtafiti amefanikiwa kuibuka na majibu ya  maswali ambayo alikuwa anayafuatilia .

Ripoti hii imebainisha kila kilichokusanywa na mtafiti na utafiti huu utatoa msaada na changamoto kwa wazalendo wa Wilaya ya Newala na wadau wa uatamaduni ili waweze kufanya jitihada  katika kuimarisha na kuendeleza utamaduni wa Wamakonde hasa katika kipengele cha ngoma  ya n,domo na bakuli.


SURA YA KWANZA

1.0  UTANGULIZI
Katika sura hii imeonyesha usuli wa mada, ufafanuzi wa mada, madhumuni ya utafiti, umuhimu wa utafiti, maswali ya utafiti sababu za kuchagua mada na vikwazo vya utafiti

1.1 Usuli  wa  Mada
Wamakonde ni   kabila moja wapo katika makabila ya Mkoa wa Mtwara na wengine hupatikana katika nchi ya Msumbiji. Katika Mkoa wa Mtwara Wamakonde wameenea Mkoa mzima ingawa wameenea zaidi katika Wilaya ya Newala, Tandahimba na Mtwara vijijini. Wamakonde wamekuwa mstari wa mbele katika kudumisha Mila na Desturi. Katika kudumisha Mila na Desturi Wamakonde hujishughulisha  na uchezaji wa ngoma, uchongaji, ufinyanzi, kilimo, uvuvi na ufugaji. Waandishi mbalimbali wamejishughulisha  kuandika na kufanya utafiti kuhusu mambo yanayohusu Wamakonde, Ngoma na Utamaduni.

Mbonde (1993) amezungumzia ngoma na shughuli nyingine zinazodumisha Utamaduni wa Wamakonde. Mnale (2012) amezungumzia ngoma kwa wakueleza namna Wamakonde walivyo cheza na kuiasa jamii kuenzi Mila, Destili na Utamaduni wetu kwa ujumla.
Ghassany (2010)amejaribu kunesha asili ya Wamakonde na kuonesha sababu ya Wamakonde wa Mtwara kuitwa Wamakonde Wamaraba. Taylor (1870) alitumia maneno ya utamaduni wa juu na wa chini kupendekeza nadharia ya ukuaji wa dini. Omari (1981) amejaribu kuzungumzia uzuri wa ngoma ya Sindimba ambayo huchezwa na Wamakonde. IPC (2005) wamezungumzia aina ya utamaduni unaoshusha hadhi ya binadamu.  Nyerere (1967) amezungumzia umuhimu wa utamaduni katika Taifa.

1.2 Ufafanuzi wa Mada
Wamakonde wanazo ngoma za namna nyingi ambazo hutumika kwa kuburudisha, kuelimisha na kuazimisha kumbukumbu fulani. Miongoni mwa ngoma zinazopatikana katika kabila la Wamakonde Wilayani Newala ni pamoja na Sindimba, Ngongoti, Singenge, Wama, Chingenge, Machenga, Bakuli, N’domo na Mchakacha. Ngoma za Bakuli na N’domo ni ngoma ambazo huwavutia watu wengi sana zinapochezwa. Kwa kiasi kikubwa ngoma ya N’domo na Bakuli zimekuwa na athari kubwa sana kwa jamii ya Wamakonde. Hapa tunazungumzia uzuri na ubaya wa ngoma hizi. Matarajio ya jamii kwa ujumla ni Kuona Mila, Desturi na Utamaduni kwa ujumla vinadumishwa ingawa kuna nguvu za mvutano zinazopelekea mambo yanayo tambulisha utamaduni wa jamii ya Wamakonde kupungua au kutoweka kabisa. Utafiti huu umechunguza athari za ngoma ya Bakuli na N’domo kwa Utamaduni wa Wamakonde hapa mambo mbalimbali yameangaliwa ambayo yanadhaniwa kuwa yanaweza kuwa  hatari kwa utamaduni wa Wamakonde.

1.3 Madhumuni ya Utafiti
1.3.1 Lengo la jumla
Kubaini athari ya ngoma ya N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde
1.3.2  Malengo Mahsusi
(a)        Kubaini ufaafu wa ngoma ya N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde.
(b)        Kubaini udhaifu wa ngoma ya N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde
(c)        Kubaini nyimbo za ngoma ya  N’domo na Bakuli
(d)       Kubaini sababu za vijana kutopenda kucheza ngoma ya N’domo na Bakuli
(e)        Kubaini mambo yanayoweza kuboresha na kuendeleza ngoma ya N’domo na Bakuli.

1.4 Umuhimu wa Utafiti
Utafiti huu unatoa changamoto kwa wadau mbalimbali wanaopenda kuendeleza Utamaduni waweze kutafutia ufumbuzi mambo yanayohatarisha ngoma ya N’domo na Bakuli. Kila anayependa kuenzi na kuendeleza utamaduni atanufaika na utafiti huu kwani umeweka wazi mambo mbalimbali juu ya ngoma za asili katika kabila la Wamakonde hasa kuhusu ngoma ya N’domo na Bakuli. Wanafunzi wa ngazi zote watanufaika na utafiti huu kwani ni nuru katika mambo yanayohusu utamaduni wa Wamakonde hasa katika kipengele cha ngoma.

1.5       Maswali ya utafiti
(a)           Ni nyimbo zipi zinazoimbwa wakati wa  kucheza ngoma ya n’domo na bakuli?
(b)           Ngoma ya n’domo na bakuli zina  ufaafu gani kwa utamaduni wa Wamakonde?
(c)           Je, ngoma ya bakuli na n’domo zina udhaifu gani kwa utamaduni wa wamakonde?
(d)          Kwa nini vijana kuanzia mika 15 hadi 39 hawapendi kucheza ngoma za asili hasa bakuli na n’domo ?
(e)           Ni mambo gani yafanyike ili kuboresha na kuendeleza ngoma ya n’domo na bakuli?


1.6       Sababu za kuchagua  mada
Mtafiti wa mada  ya Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli kwa Utamaduni wa Wamakonde  aliamua kuchagua mada hii kutokana na uzalendo wake. Mtafiti ni Mmakonde wa Newala, amebaini kuwa kizazi kilichopo hivi sasa kinaona kujishughulisha na shughuli za ngoma ni kujirudisha nyuma kiwakati na ni kujizehesha. Ngoma ya n’domo na bakuli hazijawahi kufanyiwa utafiti na kufahamika athari zake kwa utamaduni wa Wamakonde. Kutokana na sababu hizi mtafiti amesukumwa kufanya utafiti.

1.7       Vikwazo vya utafiti
Mtafiti alikosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watafiti, alikabili tatizo la usafiri na pia alikabiliana na ukosefu wa marejeo ya kutosha  ya kuweza kumwongoza zaidi katika utafiti wake.

Mtafiti hakuvunjwa moyo na vikwazo alivyokutana navyo bali alijitahidi kutafutia ufumbuzi vikwazo vilivyomkabili na hatimaye kufanikisha utafiti wake.                                                SURA YA  PILI
                                    MAPITIO YA KAZI TANGULIZI
2.0      Utangulizi
Watafiti na waandishi mbalimbali wamejishughulisha na masuala yanayohusu, ngoma, Wamakonde na utamaduni. Kila mtaalam amejaribu kuzama na kuibuka katika bahari ya utafiti na uandishi, na mtafiti wa kazi hii naye amejaribu kadri ya uwezo wake kupitia kazi hizo kwa kina ili naye aweze kubaini ukamilifu na upungufu wake ili iwe dira katika utafiti wake. Katika sehemu hii mtafiti ameonyesha yaliyoandikwa kuhusu ngoma, Wamakonde na kuhusu Utamaduni.

2.1       Yaliyoandikwa kuhusu ngoma
Mbonde (1993) anasema, “Ngoma huchezwa kwa shabaha ya kustarehesha, kuburudisha, kuadilisha, kuelimisha, kuadhimisha tamasha au kumbukumbu fulani na nyingi nyingine.” Bonuti (2000) anasema kuwa “Unapozungumzia ngoma unapata maana nyingi, kwa pamoja zinaleta  mada za aina tofauti zinazohusu dini, utamaduni, mila na desturi, siasa na historia.”  Finegan (1970) anasema kuwa “Ngoma ni ala ya muziki inayotumika sana barani Afrika, ni muziki unaochezwa na ala.” Balisidya (1987)  anasema kuwa “Kupitia ngoma tunaweza kupata nyimbo za Kishairi zenye kutumia mahadhi, melodia, mkongosio na muala.” Mulokozi (1996) anasema kuwa “Ngoma hutumia sana fomula na kauli za kimapokeo ambazo zinafahamika kwa watu wengi wa jamaii husika.” Khamis & Madumula (1989) wanauelezea utanzu huu wa ngoma kwa kusemsa kuwa “Utanzu huu haujachunguzwa kwa kiasi cha kutosha huenda ugunduzi huu wa kiafrika ukapotea bila kuacha kumbukumbu za kuridhisha kama haujafanyiwa kazi.” Anonymous (2010) anasema “Badala ya kucheza ngoma za kwetu tunaruka na salsa na rumba zisizo asili yetu. Kibaya zaidi hakuna anayejua kucheza aina hiyo ya muziki.”

Wizara ya Utamaduni wa Taifa na  Vijana (1979) wanasema “Kiwango cha utamaduni hutegemea sana kiwango cha ufundi wa kisayansi na ujuzi uliofikiwa na  jamii katika muhula maalum wa historia yake.”
Wizara ya Elimu ya Taifa (1986) wanasema kuwa “Ngoma ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa Taifa. Ngoma hizi ziliimarishwa na wazee  wa Kitanzania    wa hapo awali. Pia  ngoma hizo zilirithishwa kizazi hadi kizazi kingine. Vijana walijifunza mara nyingi ngoma zilichezwa pia wakati wa mavuno au watoto walipozaliwa. Hii ilisaidia kuimarisha uhusiano kati  ya kijiji na kijiji.

2:1:2    Yaliyoandikwa Kuhusu Wamakonde
Ghassany (2010) anasema, “Mmakonde, asili yake ni Msumbiji. Mkoa wa Kaskazini kabisa wa Msumbiji unaoitwa Cape Delgado. Ndiko walikotokea  Wamakonde. Katika  kuzaliana wengine wakavuka wakaja Mtwara. Hawa wakaitwa “Wamakonde Wamaraba. Kwa kuwa huku Tanzania wanatumia sana shikamoo, marahaba, shikamoo, marahaba” Mbonde (1973) ansema baadhi tu ya ngoma zinazopendwa sana na wamakonde wenyewe na watu wa makabila mengine ni kama zifuatazo; lipiku, lupanda, linjembe, mavuli au mngongoti kwa kiswahili.

Mnale (2012) anasema “…….. wanapocheza Wamakonde huchezesha viuno vyao kwenda sambasamba  na ngoma …”  Patachu (2012) anasema  “Wamakonde huishi kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji”

Marlin & Xander (1980) wanasema, “Wamakonde ni watu wanaozungumza kibantu ambao huishi kaskazini mwa Msumbiji na kusini mwa Tanzania.  Koo za Wamakonde zimechimbuka Msumbiji. Kutokana na uhaba wa ardhi na chakula baadhi yao waliamua kuhamia Tanzania katikati ya karne ya 20.

Finke (2000) anaamini kuwa, “ Kundi dogo la Wamakonde walihamia Kenya mwanzoni mwa karne ya 20 na walibakia huko. Walienda kufanya kazi katika mashamba ya mkonge yaliyopo kati ya mlima Kilimanjaro na vilima vya Taita ambayo yalianzishwa na wakoloni. Sifahamu kama walihamia kwa hiari au waliletwa  na wakoloni ( wajerumani au Waingereza) kama vibarua wa kulazimishwa.”

2:1:3    Yaliyoandikwa Kuhusu Utamaduni
Taylor (1870) aliyatumia maneno haya ya utamaduni wa juu na chini kupendekeza nadharia ya ukuaji wa dini. Gazeti la Express  (31/07/- 06/08/1997) wanasema, “Huu muziki unatokana na tamaduni nyingi.”  Nyerere (1967) alitamka kwamba “Nchi isiyokuwa na Utamaduni wake haina tofauti na mkusanyiko wa watu ambao hawana roho iwawezeshayo kuwa taifa.”

IPC (2005) wanasema “Ukichunguza tamaduni za jamii mbalimbali utagundua kuwa tamaduni hizo hazimuinui mwanadamu na kumfikisha katika kilele cha hadhi yake, bali kinyume chake huiteremsha hadhi yake tukufu ya ukhalifa wa Allah (S.W), kwa vile utamaduni huu umefumwa na mwenyewe Sub – Haanahu Wata’aala, mjuzi wa kila kitu, mwenye hekima.

Wizara ya utamaduni wa taifa na vijana (1979) wanasema “kiwango cha utamaduni hutegemea sana kiwango cha ufundi wa kisayansi wa historia yake. Kiwango hiki hudhihirika katika vipengele sita muhimu”  Omari (1981) anasema, “Utamaduni ni tokeo la uhusiano wa wanadamu katika maisha yao. Ni wanadamu tu ambao wana uwezo wa kuunda aina fulani ya utamaduni wa kuyamudu na kuyatosheleza matakwa yao. Masatu (1997) anasema ” Utamaduni ni jumla ya njia zote za maisha ya mwanadamu kama vile  tabia ya ulaji, wanachovaa, lugha yao, ujuzi wa, imani yao na mengineyo.”

Ndosi (2008) anaamini kuwa “ Utaratibu wa maisha au Utamaduni hurithishwa kutoka kizazi hadi kingine. Kadhalika mila na desturi za jamii hubadilika baada ya muda, hasa katika zama hizi za utamaduni” Mosha (2010) anasema kuwa “Utamaduni ni jumla ya mambo yote anayofanya binadamu kuboresha maisha yake. Mambo hayo ni pamoja na mila na desturi, elimu, tabia, kazi, dini  na imani, lugha, michezo , starehe na chakula.”

Mangwela (2008) anaamini kuwa “ Utamaduni ni jumla ya mambo yaliyobuniwa na binadamu mambo hayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya, yanaweza kudumishwa,  kuendelezwa, kuigwa au kuachwa, michezo ya jadi, ngoma za asili, nyimbo na heshima ni utamaduni unaopaswa kuigwa kudumishwa na kuendelezwa na jamii. Lakini ukeketaji wanawake ni mila potofu inayopaswa kuachwa  na jamii”.

Munisi (2011) anasema kuwa “Utamaduni  huwaunganisha na kuwakutanisha watu kuwa ni wa jamii moja. Unaweza kuwatambua watanzania kwa lafudhi yao wanapoongea lugha ya Kiswahili, pia unaweza kuwatambua wanapocheza ngoma za jadi.”

Taasisi ya Elimu Tanzania (1998) inaamini kuwa “ Utamaduni sio nyimbo au ngoma tu, bali ni mkusanyiko wa mambo mengi yanayogusa mila na desturi za Waafrika. Baadhi ya shughuli za utamaduni ni lugha za kiafrika, michezo, ngoma, nyimbo, maonyesho, mavazi, usafi, utendaji bora na matokeo ya kazi mbalimbali, ufugaji sanaa, ufundi, kuhifadhi mazao, kuamkiana kwa heshima, ndoa, mapishi na makazi ya pamoja.

2.2 Mapungufu ya Kazi Tangulizi
‘’Kiwango cha utamaduni hutegemea sana  kiwango cha ufundi wa kisayansi na ujuzi uliofanikiwa na jamii katika muhula  maalum wa historia yake’’ kiwango cha utamaduni hutegemea ufundi wa Kisayansi.
‘’Katika kuzaliana wengine wakavuka wakaja Mtwara. Hawa wakaitwa Wamakonde Wamaraba. Kwa kuwa huku Tanzania wanatumia sana shikamoo, Marahaba, Shikamoo, Marahaba”. Si kila anaye tumia shikamoo, marahaba ni Mmakonde.
‘’ Wanapocheza Wamakonde huchezesha viuno vyao kwenda sambamba na ngoma.” Si kila ngoma ya Wamakonde huchezesha viuno’’ Ngoma kama vile Bakuli na N’domo viuno havina nafasi kabisa.
‘’Koo za Wamakonde zimechimbuka Msumbiji kutokana na uhaba wa ardhi na chakula baadhi yao waliamua kuhamia Tanzania katikati ya karne  ya 20.’’ Uhaba wa chakula na ardhi sio sababu iliyowafanya baadhi ya Wamakonde kuhama Msumbiji na kuhamia Tanzania bali walisukumwa na vita nchini Msumbiji na kuvutiwa na amani nchini Tanzania.

2.3 Kitu Kipya Kilichooneshwa katika Utafiti huu.
Utafiti huu umeonesha ufaufu na udhaifu wa ngoma ya N’domo na Bakuli kwa Utamaduni wa Wamakonde, nyimbo zinazoimbwa wakati wa kucheza ngoma N’domo na Bakuli, sababu zinazopelekea vijana kutopenda kucheza ngoma za asili hasa ngoma ya N’domo na Bakuli na mambo yanayoweza kuboresha bakuli na mambo yanayowezakurekebisha na kuendeleza ngoma za N’domo na Bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde.

                                              SURAYA TATU
                                           MBINU ZA UTAFITI
3.0       Utangulizi
  Sura hii imeonyesha mambo mbalimbali ambayo ni pamoja na mbinu za utafiti, mpango wa utafiti, eneo la utafiti, walengwa wa utafiti,mbinu za ukusanyaji data,mbinu za uchambuzi wa data na udhibiti wa data.

3.1 Mpango wa Utafiti
Mtafiti alikusanya data katika  kata ya Chihangu na Mnyambe ambapo vijiji vya Mtongwele, Meta, Chihangu, Bahati,Mnayope na Mnyambe vimetembelewa na mtafti katika wilaya ya Newala, mtafiti alitumia muda wa siku 6 katika kukusanya data ambapo alikusanya kwakutumia mahojiano (maelezo) ya ana kwa ana,na madodoso. Mtafiti katika maeneo yote aliyotembelea alilenga kukusanya data juu ya nyimbo ya ngoma ya n’domo na bakuli,ufaafu wa ngoma ya n’domo na bakuli, udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde, sababu za vijana kushiriki katika uchezaji wa ngoma ya n’domo na bakuli na mbinu za kuboresha ngoma ya ndomo na bakuli. Mtafiti amefanikiwa kupata majibu ya vipengele vyote, pia amesoma vitabu mbalimbali ambavyo vimezungumzia habari za Wamakonde , utamaduni na ngoma

3.2 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika mkoa wa Mtwara ambao una Wilaya tano (5) na halmashauri sita (6) ambazoni Masasi, Nanyumbu, Newala ,Tandahimba, Mtwara mjini na Mtwara vijijini, Tarafa 25, kata 149, vijiji 738, vitongoji 3126, na Mitaa 85. Mkoa wa Mtwara una makabila makuu matatu ambayo ni Wamakonde,Wayao,Wamakuwa( Jumanne .I. :2013) . Kwa mujibu wa mzee Nailoni (2013) alisema “Kihistoria makabila haya, hapo awali waliishi pamoja na makabila mengine kaskazini mwa mto Ruvuma. Makabila haya yaliacha makabila yao na kukimbilia Msumbiji, kutokana  na vita vya makabila kutoka kaskazini mwa Tanganyika. Katika kuishi Msumbiji amani na utulivu vilitoweka kutokana  na vita vya Wazulu. Makabila hayo yakarudi ng’ambo ya mto Ruvuma.

Mtafiti amekusanya data katika kata mbili za wilaya ya Newala ambazo ni kata ya Chihangu na Mnyambe ambazo zina vijiji vilivyotajwa kipengele cha 3.1 hapo juu katika tarafa ya Chilangala. Katika kukusanya data mtafiti alitembelea shuleni, nyumbani kwa wadau mbalimbali wanaojihusisha na wasiojihusisha na shughuli za uchezaji ngoma.

Sababu zilizo mfanya mtafiti kuchagua eneo hili ni pamoja na:-
·         Muda wa kukusanya kuchanganua data na kuandika ripoti ulikuwa mdogo
·         Mtafiti alikosa fedha za kutosha za kumwezesha kuchukua eneo kubwa.
·         Ni eneo ambalo mtafiti amekulia na kusomea kwa hiyo analifahamu vizuri.
·         Ndio maeneo ambayo ngoma ya n’domo na bakuli zimeshamili zaidi

3.3 Walengwa wa Utafiti
Utafiti huu uliwahusu Wamakonde wa wilaya ya Newala Mkaoni Mtwara.Wamakonde waliopo Newala inasemekana waliingia nchini Tanzania mwanzoni mwa karne ya 20 wakitokea Msumbiji kukimbia vita vilivyokuwa vinapigwana huko. Wamakonde katika kuendeleza utamaduni wao hujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile Kilimo, Uvuvi, Uchongaji,Uhunzi,Ufinyanzi, Ufugaji,nauchezaji ngoma

Katika shughuli zao kwa kiasi kikubwa huzifanya kwa ushirika, kwamfano katika shughuli za kilimo wanalima kwa njia ya chama au mkumi.Wamakonde wamegawika katika koo mbalimbali kama vile Nahonyo, Mtanda, Mwaya, Mbonde, Meta, Chihangu, Munga, Namangaya, Nanyanje, na Mpwapwa..  Koo hizi hushirikiana katika shughuli mbalimbali kwa njia ya utani, kwamfano Mtanda wakifiwa huwaalika ukoo wa Mbonde kuja kuzika ambapo hutoa mahitaji mbalimbali ya kukamilisha mazishi.

3.4              Watafitiwa
Utafiti huu uliwahusisha wazee na vijana, wasanii, walimu, wanafunzi na wasio wasanii wakike na wakiume wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 80. Watafitiwa wamepatikana katika njia kuu mbili ambazo ni njia ya kukusudia na njia ya bahati nasibu.

Wasanii: Kundi hili limejumuisha wapigaji ngoma, wachezaji na watunzi wa nyimbo. Kundi hili limechaguliwa kwasababu wao ndio wahusika wakuu wa ngoma.

Wazee: kundi hili limechaguliwa kutokana na uzoefu wao katika maisha kwani kuishi kwingi ni kuona mengi pia wazee ndio wahusika katika uchezaji wa ngoma ya n’domo na bakuli.

Washabiki: Hawa wamechaguliwa kutokana na upenzi wao katika kuangalia ngoma zinapo chezwa kwahiyo mtafiti aliamini atapata taarifa nyigi kutoka kwao.

Vijana: Kundi hili liliteuliwa kutokana na kujitenga kwao na uchezaji wa ngoma za asili

Wasomi: Kundi hili nalo lilipewa kipaumbele kutokana na ufahamu wao wa mambo mbalimbali katika jamii hasa kuhusu suala la utamaduni.
Kutokana na sababu za watafitiwa waliotajwa hapo juu mtafiti alifanikiwa kupata data tena kwa haraka makundi yote yalichaguliwa kwa kuzingatia jinsia zote mbili,jumla ya watafitiwa walikuwa 60. Ufafanuzi zaidi ni kama ulivyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo hapo chini:

Jedwali 1: kategoria za wahojiwa

KATEGORIA/ WAHOJIWA
WANAWAKE
WANAUME
JUMLA
ASILIMIA
WASANII
01
05
6
10%
WAZEE
04
12
16
27%
WASHABIKI
07
09
16
26%
VIJANA
05
05
10
17%
WASANII
03
09
12
20%3.5              Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu ulijihusisha na athari za ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde. Mtafiti alijishughulisha na utafiti wa nyimbo za ngoma ya n’domo na bakuli,ufaafu na udhaifu wake, sababu za vijana kutopenda ngoma za asili na mbinu zinazoweza kutumika kuendeleza ngoma za asili wilayani Newala kwa utamaduni wa wamakonde.
Mtafiti hakujihusisha na asili ya ngoma ya  n’domo na bakuli, sababu ya kuitwa majina haya na mavazi yanayo valiwa wakati wa kucheza ngoma hizi.


3.6              Zana  na Vifaa vya Utafiti
Katika kukamilisha utafiti huu mtafiti ametumia zana na vifaa mbalimbali kama vlie, kalamu kwa kuandikia, karatasi kwa ajili yakutunza kumbukumbu, Simu kwa mawasilano, kinasa sauti kwa kunasia sauti, madodoso, hojaji na durusu ya maandiko.
3.7              Mbinu za Ukusanyaji wa Data
Katika kukamilisha utafiti huu mtafiti alitumia madodoso, hojaji, uzoefu wa mtafiti na ugunduzi makini.3.7.1        Dodoso
Mtafiti aliandaa dodoso za aina mbili ambazo ni dodoso la vijana kuanzia miaka 15 hadi 39 na la watu wazima wenye umri wa miaka 40 hadi 80.Dodoso ziligawiwa kwa watu hamsini na nne (54) maswali yalikuwa ni ya wazi na funge.

3.7.2        Hojaji
Mtafiti alitumia hojaji yenye maswali 6 (sita ) ambapo wahojiwa 6 (sita ) walihojiwa  ambao ni wazee ambao hawawezi kusoma na kuandika. Hawa walikuwa na uzoefu mkubwa katika ngoma ya n’domo na bakuli ndio maana mtafiti aliona bora atumie njia hii hata kama hawajuwi kusoma na kuandika mbinu hii iliwawezesha kutoa uzoefu wao.
3.7.3        Ugunduzi makini
Katika kukusanya data mtafiti alitembelea maeneo mbalimbali ambako wachezaji ngoma ya n’domo na bakuli wanaishi na alijionea vifaa na zana mbalimbali zinazotumika katika uchezaji ngoma ambazo ni pamoja na njuga, makuti, filimbi na makungwa  na indunda. Ingawa mtafiti hakubahatika kushuhudia ngoma hizi zikichezwa wakati wa anafanya utafiti

3.7.4        Uzoefu wa Mtafiti
Mtafiti kwa kiasi kikubwa aliongozwa na uzoefu wake katika kufanya utafiti huu, kwani yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Mtongwele II Wilayani Newala na amesoma shule ya msingi katika kijiji hicho na elimu ya sekondari amesoma shule ya Mnyambe.Maeneo haya yote aliyopitia mtafiti  ndio maeneo ambayo ngoma hizi zilikuwa zikichezwa kwa hiyo mtafiti alikuwa anafahamu kabla ya kuamua kufanya utafiti.


3.8              Udhibiti wa Data
Mtafiti katika kuhakikisha uasili na usahihi wa data katika ukusanyaji  na uwasilishaji wake alisambaza  madodoso na alisimamia yeye mwenyewe ili kuhakikisha watafitiwa wametowa taarifa za kweli na alichagua watu makini walio wakweli na wanaojua umuhimu wa utafiti na aliwaelimisha kabla  ya kutoa taarifa zao. Alipotumia njia ya hojaji mtafiti alitumia mahojiano ya ana kwa ana lakini pia ikumbukwe kuwa mtafiti alitumia uzoefu wake katika kutoa mwongozo katika upatikanaji wa taarifa sahihi.Katika kufanya udurusu wa maandiko mtafiti alijitaidi kupitia vitabu vyenye ithibati kubainisha taarifa za kitabu hicho kama vile, nani kasema,mwaka gani, na nani amechapa3.9              Mbinu za Uchanganuzi wa Data
Data zilizopatikana mtafiti aliziwasilisha kwa njia ya maelezo ambapo alitumia majedwali na alionesha kwa asilimia pale panapohusika.
                                               SURA YA NNE
                                          TAARIFA ZA UTAFITI

4.0              Utangulizi
Sehemu hii imeshughulikia data zilizokusanywa wakati wa utafiti. Mtafiti amekionesha kila alichokutana nacho wakati wa utafiti wake.Sehemu hii ina vipengele mbalimbali ambavyo ni pamoja na uwasilishaji wa data na uchanganuzi wa data na kipengele cha mjadala.

4.1              Uwasilishaji wa data
4.1.1    Majibu ya madodoso kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 39
4.1.1.1 Faida  za ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde
·         Kuendeleza utamaduni wa wamakonde
·         Mazoezi ya mwili
·         Kufurahisha jamii
·         Kukuza mshikamano
·         Kuelimisha jamii
·         Kupunguza uzururaji
·         Kuendeleza amani na upendo katika jamii
·         Kuondoa matabaka katika jamii
·         Hazina faida
·         Sijui
·         Kuendeleza ushirikina

4.1.1.2.1        Miongoni mwa madhara ya kushiriki katika ngoma ya n’domo na Bakuli ni pamoja na:-
·         Kuumwa mafua kutokana na vumbi wakati wa kucheza
·         Kupoteza muda bila sababu maalumu
·         Kuharibika Kisaikolojia
·         Malumbano
·         Kulewa bila ya kujitambua
·         Kumsahau Mungu
·         Ubakaji
·         Ugomvi
·         Uvivu wa kufanya kazi
·         Huchezwa usiku
·         Kuenea kwa umalaya
·         Kukosa kufanya mambo ya maendeleo
·         Utakosa kudumisha na kuboresha maisha
·         Kudumaza akili
·         Sehemu zenye mikusanyiko ya watu kuna madhara mengi
·         Watoto wa kike kupata mimba
·         Kuchomana visu
·         Kutokwenda shuleni wanafunzi
·         Kudumaza Watoto
·         Watoto wadogo kukosa elimu
·         Kuwapotosha wanafunzi
·         Kupata magonjwa

4.1.1.3    Sababu ya vijana kutopenda kucheza ngoma  ya n’domo na bakuli
·         Wanaona mambo ya zamani
·         Wanaona hazina faida
·         Zinawapotezea muda wa kufanya mambo ya kimakonde
·         Hazina maana yoyote kwao
·         Kujisikia aibu
·         Husema wanakwenda na wakati
·         Kuzungukwa na tamaduni za kigeni
·         Kutokana na athari za tamaduni
·         Kutojua maana ya ngoma ya asili
·         Kutojua umuhimu wa ngoma za asili
·         Wanaona aibu
·         Huona kama wanaharibu maadili
·         Huona kama wanapoteza muda
·         Kutopenda utamaduni wetu
·         Kutoshirikiana na wakongwe
·         Wanaiga utamaduni wa nje
·         Wengi huishi mjini ambako si rahisi kuzikuta
·         Uhaba wa elimu ya uraia
·         Kwasababu sijawahi kuiona
·         Kukosa muda wa kujiandaa na maisha
·         Zimekufa muda mrefu
·         Kukosa muda wa kujiandaa na maisha
·         Vijana wanaona wanachelewa kazi zao
·         Zina hasara kwa vijana
·         Kuna mambo yasiyo jenga
·         Ni ngoma za wazee
·         Kushamili kwa matusi

4:1:1:4 Mambo yanayoweza kuboresha na kuendeleza ngoma ya n’domo na Bakuli.
·         Serikali itoe elimu juu ya ngoma za asili
·         Vijana waunde vikundi vya ngoma za asili
·         Kuondoa aibu kwa vijana
·         Kutoacha kucheza ngoma za asili
·         Kujali mila na Destuli zetu
·         Kuboresha mavazi ambayo yanavaliwa wakati wa kucheza ngoma
·         Pasiwepo na malumbano
·         Wapenzi na washabiki
·         Vifaa vya ngoma viletwe na wafadhili
·         Kupanda miti ya kuchonga ngoma
·         Upatikanaji wa ngozi
·         Kucheza bila kupigana
·         Kuanzisha bendi
·         Ngoma ziwe na mshikamano mmoja
·         Kuelimisha jamii juu ya utamaduni
·         Kutoa maelezojuu ya umuhimu wa ngoma za asili
·         Kufuga wanyama kwa ajili ya ngozi
·         Serikali itoe misaada katka vikundi vya ngoma

4.1.2          Majibu ya Madodoso ya Wazee wenye Umri wa Miaka 39- 80

4.1.2.1  Faida za Ngoma ya N’domo na Bakuli
 • Zinafurahisha jamii
 • Watu wanapenda kusikiliza na kucheza
 • Zina vichekesho vingi katika jamii
 • Huifanya jamii iwe na amani na upendo
 • Huunganisha familia mbalimbali
 • Huondoa tofauti mbalimbali zilizopo katika jamii
 • Hufurahisha watu
 • Huburudisha
 • Hudumisha ngoma za asili
 • Kulinda utamaduni
 • Kurithisha mila na destuli
 • Kuendeleza kijiji
 • Kukaribisha wageni wa serikali
 • Kuendelea kijiji
 • Kukaribisha wageni wa nchi za nje
 • Mazoezi ya viungo
 • Huleta umoja katika jamii
 • Hudumisha ushirikiano katika shughuli mbalimbali
 • Nyimbo nyingi ni za mafunzo kwa jamii
 • Kupata sehemu za kupumzika
 • Kupata fedha za kujikimu
 • Kupata mwenza
 • Kupata wasanii

4:1:2:2 Udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde.
 • Kurudisha nyuma maendeleo
 • Kupoteza muda wa maendeleo
 • Kuenea kwa magonjwa
 • Kushuka kwa uchumi
 • Kuongezeka kwa ulevi katika jamii
 • Kushamiri kwa uzinifu
 • Kuenea kwa ulevi
 • Husababisha ugomvi
 • Huchangia mimba za utotoni
 • Hudumaza akili
 • Hupoteza muda wa kushughulikia mambo ya msingi
 • Huleta  uwezekano wa maambukizi ya mdomo
 • Maambukizi kwa vyombo vichafu
 • Haina vichochezi kwa watumiaji


                                                                                                                                                     4.1.2.3  Madhara ya Ngoma ya N’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde
·         Husababisha ugomvi
·         Hudumaza akili
·         Kurudisha nyuma maendeleo ya jamii
·         Kutengwa na viongozi wa dini
·         Wanaocheza ngoma huitwa makafili
·         Huwapotezea waumini muda wa kufanya ibada
·         Kushamili kwa ulevi
·         Hupelekea mmomonyoko wa maadili

4.1.2.4 Nyimbo zinazoimbwa wakati wa kucheza ngoma ya N’domo na Bakuli

4.1.2.4.1 Nyimbo za ngoma ya N’domo  
            Chivamando kuvipedo eee ooo x2
            Kiitikio: Chivamando kuvipedo oo
            Ndoo ndoo mwinamaa oo mwinama x2
            Kiitikio: Ooo mwinamaa

            Naliyela oo x2
            Kiitikio: Oo liyele

            Serikali ya namwaka kulipembejaa x2
            Kiitikio: Oo kulipembejaa

4.1.2.4.2 Nyimbo za ngoma ya Bakuli
Kunkoma kwa Nangololo waislamu wamekula nditi x2
Kiitikio: Pombe haramu ee

Bakuli ee bakuli x2
Kiitikio: Ukanaandike bakuli kulandana

Ayu mwene ingole nani ooo mm x2
Kiitikio: Ayu nangolo oo

Chiwowa wowa woo woo x2
Kiitikio: Tulambilana nkanya oo
Mchawi kuroga litingi nannuku nwaliya x2
Kiitikio: Nannuku nwaliya ooo

Chii chii chinanganga avetu vahwena x2
Kiitikio: Chii chinanganga

4.1.3          Majibu ya hojaji
4.1.3.1 Mchango wa ngoma ya N’domo na Bakuli kwa Utamaduni wa Wamakonde
 • Kuendeleza utamaduni
 • Kuendeleza Utamaduni
 • Kuelimisha jamii
 • Kuleta kipato katika kikundi cha ngoma
 • Kurithisha Mila na desturi za Wamakonde
 • Kukemea tabia mbaya katika jamii
 • Kujenga undugu na mshikamano katika jamii

     4.1.3.2  Sababu za Vijana Kutopenda Kushiriki katika Uchezaji wa Ngoma ya N’domo na Bakuli
 • Kwenda na wakati
 • Kupoteza muda
 • Kuona aibu
 • Ngoma zimepitwa na wakati
 • Athari za utandawazi
 • Hawapati kipato
 • Hawapendi mambo ya kiutamaduni
 • Athari za dini
 • Kuwadharau wazee
 • Wanapenda muziki
 • Hawachezi Shuleni

4.1.3.3 Mambo yanayoweza kuboresha Ngoma ya N’domo na Bakuli
·         Katika maazimisho ya Kitaifa ngoma hizi zipewe kipaumbele
·         Vyombo vya habari vitumike katika kuvitangaza vikundi vya ngoma hizi
·         Mafunzo ya Ngoma yaanzie Shuleni
·         Watoto jandoni na unyagoni wafundishwe Ngoma hizi
·         Serikali itoke misaada
·         Serikali itoe ajira kwa wachezaji ngoma hizi
·         Vikundi vya Ngoma viwe vya uzalishaji mali

4.2.1 Ngoma ya N’domo
Ngoma hii ni ngoma maarufu sana kwa wazee wa Kimakonde na huchezwa na watu wazima wakike na wakiume kuanzia umri wa miaka 40 na kuendelea. Ngoma hii huchezwa wawili wawili huku wachezaji wakiwa wanatazamana na watu wengine huwa wanapiga makofi na kuimba huku Ngoma zikipigwa.Ngoma hii huwa wanafungana au kulana ambapo mchezaji anatakiwa apeleke mguu wake kinyume na mguu wa mwenzake akipeleka sambamba na mguu wa mwenzake huwa amefungwa na huondolewa na kuingia mwingine.

Nyimbo zinazoimbwa wakati wa kucheza n’domo huwa ni za kubuni kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea katika jamii kwa mfano Mtu akilewa na kufanya maovu wimbo unaweza kutungwa ili kumkemea. Kwa mujibu wa Mzee Amiri Chimbanga wa Mtongwele (2013) alisema kuna watu wa Mkoma walilewa pombe kisha wakamla nditi (Ndege Ngoma) ambaye waislamu hawaruhusiwi kumla wimbo ukatungwa ili kuwakemea kama ifuatavyo:-
            Kunkoma kwa nangalolo Waislamu wamekula nditi x2
            Kiitikio: Pombe haramu ee     
             

Madodoso ya wahojiwa 54 ambao ni 90% ya wahojiwa wote na majibu ya hojaji 6 sawa na 10% za wahojiwa wote katika  kuelezea ufaafu wa ngoma ya n’domo na bakuli waligawanyika makundi matatu kama kielelezo hapo chini kinavyoonyesha.

Jedwali namba 2: makundi ya ufaafu wa ngoma

WALIOHOJIWA
IDADI
ASLIMIA
HAZINA  UFAAFU
10
17%
SIIFAHAMU NGOMA YA N’DOMO WALA BAKULI
20
33%
ZINA UFAAFU
30
50%
JUMLA
60
100%Kwa mujibu wa kielezo hapo juu wahojiwa 10 sawa na 17% walisema ngoma ya n’domo na bakuli hazina ufaafu wowote, wahojiwa 20 sawa na 33% walisema hawazifahamu ngoma ya n’domo na wahojiwa 30 sawa na 50% walisema zinaufaafu mkubwa na ufaafu wao uligawika makundi mbalimbali kama kielezo chini kinavyoonesha .

Jedwali 3: Mgawanyo wa Majibu ya Ufaafu wa Ngoma  ya N’domo na Bakuli

MGAWANYO WA MAJIBU
IDADI
ASILIMIA
UFAAFU KISIASA
8
16%
UFAAFU WA KIJAMII
24
49%
UFAAFU WA KIUTAMADUNI
14
29%
UFAAFU WA KIUCHUMI
3
6%
JUMLA YA MAJIBU
49
100%

        
Kutokana na majibu hapo juu katika kielelezo inaonesha kuwa ngoma ya n’domo na bakuli  zinaufaafu zaidi kijamii kwa 49% na kufuatia kiutamaduni kwa 20% na mwisho ni kisiasa 16% na kiuchumi kwa 6% .
Madodoso ya watafitiwa 54 ambao ni sawa na 90% na wahojiwa 6 sawa na 10% majibu yao juu ya sababu za vijana kutopenda kucheza ngoma za asili hasa  ngoma ya n’domo na bakuli yaligawika katika makundi 9 kama ifuatavyo katika kielelezo.
Jedwali namba 4: Sababu za Vijana Kutopenda Ngoma
MGAWANYO WA MAJIBU
IDADI YA MAJIBU
ASILIMIA
HAINA FAIDA
7
16%
KUTOFAHAMU UMUHIMU
6
17%
KUONA AIBU
5
11%
ATHARI ZA DINI
5
11%
KUHAMAHAMA
2
16%
ZIMEPITWA NAWAKATI
7
4.5%
INAMOMONYOA MAADILI
4
9%
UTANDAWAZI/ UMAGHARIBI
5
11%
SIJAWAHI KUIONA
2
4.5%
JUMLA
44
100%


Kielelezo cha hapo juu kinaonesha sababu mbalimbali zinazopelekea vijana kutopenda kucheza ngoma za asili hasa ngoma ya n’domo na bakuli. 16%  hazina faida kwa vijana, 18.5% walisema ngoma za asili zimepitwa na wakati,  13.5% walisema kwasababu ya utandawazi na umagharibi, 17% kutokana na kutofahamu umuhimu wake, 9%  zinamomonyoa maadili ya jamii, 11% vijana wanaona aibu, 11% wengine walisema ni kutokana na athari za dini, 4.5% kwasababu vijana hupenda kuhamahama na 4.5% wengine walisema hawajawahi kuziona ngoma ya n’domo na bakuli.
Madodoso ya wahojiwa 54 ambao ni sawa na 90% ya wahojiwa wote katika majibu yao ya kueleza udhaifu / madhara ya kushiriki katika uchezaji wa ngoma ya n’domo na bakuli yaligawika katika mafungu matano kama ilivyoonyeshwa katika kielelezo kifuatacho.Jedwali Namba 5: Udhaifu wa Ngoma  ya N’domo na Bakuli
MAKUNDI YA MAJIBU
IDADI YA MAJIBU
ASILIMA
MMOMONYOKO WA MAADILI
10
267%
KUDUMAZA MAENDELEO
8
21%
KUHARIBU WANAFUNZI
7
18.5%
KULETA UGOMVI KATIKA JAMII
6
16%
MADHARA KIAFIA
7
18.5%
JUMLA
38
100%


Kielelezo cha hapo juu kinaonyesha kwa mujibu wa majibu yaliyotolewa na wahojiwa ngoma ya n’domo inamadhara makubwa sana katika jamii ambapo huchangia mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa 26% kudumaza maendeleo 21%,kuharibu wanafunzi 18.5% madhara kiafya 18.5% na kuleta ugomvi katika jamii 16%.
Majibu ya waliohojiwa kwa kutumia hojaji ambao ni wazee 6 sawa na 10% walisema ngoma ya n’domo na bakuli hazina udhaifu wowote hali zina ufaafu tu.
Madodoso ya watafitiwa 54 sawa na 90% na majibu ya hojaji za wazee 6 sawa na 10% kuhusu mambo yanayoweza kuboresha ngoma ya n’domo yaligawika katika makundi 7(saba) kama kielelezo kinavyoonyesha hapo chini.

Jedwali 6: Mambo Yanayoweza Kuboresha Ngoma ya N’domo na Bakuli
MGAWANYO WA MAJIBU
IDADI YA MAJIBU
ASILIMIA
Serikali itoe msaada
3
13%
Itolewe elimu
6
26.5%
Vifaa vipatikane kwa urahisi 
3
13%
Kutumia maazimisho ya ya kitaifa
3
13%
Kuaandaa vikundi
3
13%
Kudumisha madili 
4
17%
Kuondoa aibu kwa vijana 
1
5%
JUMLA
23
100%


Kielelezo hapo juu kinaonesha mgawanyo wa mbinu/mambo ambayo yakifanyiwa kazi yataboresha na kuendeleza ngoma ya n’domo 26.6% walisema elimu itolewe kwa wanajamii, 17% maadili ya boreshwe katika uchezaji ngoma,13% serikali itoe misaada, 13% vifaa vipatikane kwa urahisi,13% kutumia maazimisho ya kitaifa kuboresha ngoma, 13% kuunda vikundi na 5% walisema vijana waondowe aibu.
4.2.2 Ngoma ya Bakuli
Ngoma hii huchezwa nawatu mchanganyiko yaani wanaume na wanawake ambapo wakati wa kucheza ngoma hii wachezaji husimama kwa kuunda duara na uchezaji wake huwa ni wa kuchezesha mikono na baadaye mikono hubana tumboni haya yote hufanyika huku ngoma zikipigwa na nyimbo zikiimbwa. Kwa majibu ya Bi Mariamu Binti Khamis (2013) wa Mtongwele anasema kuna wimbo maarufu ambao kila bakuli inapochezwa lazima himbwe nao ni huu ufuatao:

Bakuli Bakuli ee Bakuli x2
Kiitikio Ukanaandike bakuli kulandana
Wimbo huu unahimiza umuhimu wa kuweka alama kifaa chako ili haya kikichanganyika na vya wengine usiweze kupoteza.
Majibu ya madodoso ya hojaji kuhusu ngoma ya bakuli yanawiana na maelezo yaliyotolewa katika kipengele cha 4.2.1 kwani ngoma hizi ziliunganishwa pamoja na hata majibu yake yalifanana nay ale ya ngoma ya n’domo. Kwa maelezo zaidi rejea kielelezo namba 1 hadi namba 6
4.2                Mjadala
Utafiti huu umekusanya data kutoka kwa watafitiwa 60. Data hizi zimepatikana kwa kutumia mbinu ya madodoso, hojaji na uzoefu wa mtafiti. Kati ya watafiti 60, wazee walikuwa 16 sawa na asilimia 27%,washabiki 15 sawa na 26% wasomi 12 sawa na 20% na vijana 10 sawa na 17%.
4.3.1 Ufaafu wa ngoma ya Ndomo na Bakali kwa utamaduni wa Wamakonda. Majibu ya madodoso 54  sawa na 90% na majibu ya hojaji za wazee 6 sawa na 10% kuhusu ufaafu wa ngoma ya Bakuli na N’domo yalionesha kukili kuwepo kwa ufaafu ambapo uligawanywa katika makundi 4 ambayo ni kisiasa majibu yalikuwa 8 sawa na 16%, kijamii majibu 24 sawa na 49%, kiutamaduni majibu yalikuwa 14 sawa na29% na majibu 3yalionyesha ufaafu kiuchumi sawa na 6%.
Majibu haya ya Watafiti yanaenda sambamba na baadhi ya durusu za maandishi zilizoonyeshwa. Mbonde (1993) anasema ‘’ ngoma huchezwa kwa shabaha ya kustarehesha,kuburudisha, kuadilisha, kuelimisha, kuadhimisha tamasha au kumbukumbu Fulani ‘’ Wizara ya Elimu ya Taifa (1986) ‘’ Wanasema pia ngoma hizo zilikuwa na shabaha ya kurithisha mila na destuli kutoka kizazi hadi kizazi kingine’’ yaliyosemwa na Mbonde (1993) na Wizara ya Elimu ya Taifa (1986) ndiyo yalisemwa na Watafiti wa
4.3.2 Udhaifu wa Ngoma ya N’domo na Bakuli
Watafiti waliojaza madodoso 54 sawa na 90% ya Watafiti wote na wahojiwa 6 sawa na 6% waliohojiwa walitoa majibu mbalimbali. Mgawanyo wa majibu ya Watafiti 54 sawa na 90% yalikuwa kumomonyoa maadili katika jamii, majibu yalikuwa 10 sawa na 26% kudumaza maendeleo majibu 8 sawa na 21% kuaribu wanafunzi majibu 7 sawa na 18.5%, madhara kiafya majibu 7 sawa na 18.5% na majibu 6 sawa na 16% walisema zinaleta ugomvi katika jamii. Na wahojiwa 6 sawa na 10% walihojiwa na kutumia hojaji walisema ngoma hizi hazina udhaifu.

Yaliyojitokeza katika majibu ya Watafitiwa na nathibitisha yale yanayosemwa na waandishi mbalimbali  kwa mfano Mangwela(2008) anasema, ‘’Utamaduni ni jumla ya mambo yanayo buniwa na Binadamu. Mambo hayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya, yanaweza kudumishwa, kuendelezwa, kuigwa au kuachwa mfano, michezo ya jadi, ngoma za asili, nyimbo na heshima.

4.3.3 Sababu za Vijana kutopenda kucheza Ngoma za N’domo
Watafiti wote 60 wa dodoso 54 sawa 90% na 6 wahojaji sawa na 10% walikiri kuwa ni kweli Vijana hawapendi kushiriki katika uchezaji wa Ngoma za asili hasa  Ngoma ya N’domo na Bakuli sababu ziligawika makundi 9 ambayo ni pamoja na majibu 7 sawa 16% walisema hazina faida majibu 6 sawa17% walisema hawafahamu umuhimu wake 5 sawa 11% walisema wanaona aibu majibu 5 sawa 11% walisema athari za dini 5 sawa 11% Utandawazi/Umagharibi 7 sawa 16% zimepitwa na wakati 4 sawa na 9% zinamomonyoa maadili,2 sawa na 4.5% kuhamahama na 2 sawa na 4.5% walisema hawajawai kuona ngoma ya N’domo wala Bakuli.
Kitendo cha Vijana kutopenda kushiriki katika ngoma za asili hasa katika huchezaji ngoma ya N’domo na Bakuli hata waandishi mbalimbali wameyazungumzia. Ananymous (2010) anasema ‘’ badala ya kucheza ngoma za kwetu tunaruka na salsa na rumba zilizo asili yetu. Kibaya zaidi ni kuwa hakuna anayejua kucheza aina hiyo ua muziki.

4.3.4 Mambo yanayoweza kuboresha na kuendeleza Ngoma ya N’domo ya N’domo na Bakuli
Khamis & Madumula (1989)wanasema, ‘’Utanzu huu wa ngoma kwa kusema kuwa utnzu haujachunguzwa kiasi cha kutosha na huenda ugunduzi huu wa Kiafrika ukapotea bila kuacha kumbukumbu za kurithisha kama haujafanyiwa kazi’’ Maneno haya yanaonyesha uhusiano kati ya yale yaliyosemwa na Watafitiwa nay ale yaliyo andikwa kwani kinachosisitizwa ni kuendeleza na kuboresha kwa ngoma zetu.    

SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.0       Utangulizi
Sura hii inahusu majumuisho ya jumla juu ya tatizo la utafiti ambapo imegawanywa katika vipengele vya muhtasari, Hitimisho na hatimaye mapendekezo

5.1       Muhtasari
            Utafiti huu lilikuwa kutafiti athari za ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde. Utafiti huu umefanyika katika kata za Chihangu na Mnyambe katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara. Utafiti huu uliwahusisha wakoji wa 60 ambao ni watu 6, wazee 16, washabiki 15, vijana 1o na wasomi 12. Wahojiwa hao wote walipatikana kwa njia ya bahati nasibu na kukusudia

Vipengele vilivyotafitiwa ni pamoja na ufaafu wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde. Nyimbo za ndomo na za ngoma ya bakuli, udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli, sababu za vijana kutpenda kucheza ngoma za asili na mambo yanayoweza kuaboresha  na kuendeleza ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde.

Katika kukusanya data mtafiti ametumia  ametumia mbinu mbalimbali kama vile; uzoefu wa mtafiti, dodosona hojaji. Mbinu ya hojaji ilitumika kwa wazee 6 ambao hawajui kusoma na kuandika na mbinu zingine zilitumika kwa makundi yote ya wahojiwa.

Mapitio ya muandishi yaliyopitiwa na mtafiti kabla ya kufanya utafiti wake yanaonesha kuwa  hakuna aliyewahi kufanya utafiti juu ya mada hii. Malengo ya utafiti huu yamefanikiwa ambayo yalikuwa:-
·         Kubaini ufaafu wa ngoma ya n’domo na bakuli
·         Kubaini udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde
·         Kubaini nyimbo za ngoma ya n’domo na bakuli
·         Kubaini sababu za vijana kutopenda kushiriki kucheza ngoma ya n’domo na bakuli
·         Kubaini mambo yanayoweza kuboresha na kuendeleza ngoma yan’domo na bakuli.
Wakati wa kufanya utafiti huu mtafiti alikutana na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa marejeo ya kutosha, mwitikio mdogo kwa watafitiwa na tatizo la usafriri. Mtafiti aliweza kukabiliana na changamoto hizi kwa kuwaeleza watafitiwa umuhimu wa utafiti, baada ya kuelewa walitoa msaada mkubwa sana kwa amtafiti mpaka akakamilisha malengo yote.

Mbinu zilizotumiwa na mtafiti zimeleta matokeo mazuri kiasi ambacho kila anayetakakufanya utafiti anawezakutumia mbinu hizi. Mbinu zilizotumiwa na mtafiti kutatua changamoto zilizomkabili pia inawezakutumiwa na watafiti wengine kwani elimu ni ufunguo wa mambo mbalimbali. Jamii nayo itanufaika na utafiti huu kwani watajiepusha na mambo yanayoleta udhaifu katika ngoma na watayatumia mambo yanayowezakuboresha ngoma yaliyoibuliwa na utafiti huu.

5.2 Hitimisho
Utafiti huu umegundua kuwa ngoma ya n’domo na bakuli zina athari chana na hasi kwa utamaduni wa Wamakonde. Kutokana na kuwepo kwa athari mseto katika jamii wanajamii hawanabudi kuboresha ngoma kwa kuepukana na mambo yote yanayopelekea kutokea kwa udhaifu kama vile kucheza wakati wa usiku, wakati wa ibada au wakati wa kazi au masomo. Mtafiti pia amegundua kuwa ngoma hizi zinaanza kutoweka katika baadhi ya vijiji vilivyotembelewa na mtafiti jambo ambalo ni hatari kwa utamaduni wa wamakonde. Watafiti na waandishi wengi kwa vile wanaamini kuwa ngoma ni kipengele kimojawapo katika utamaduni ambacho kimebuniwa na wanadamu, ambacho maudhi yake yanaweza kuwa mabaya ua mazuri, yanaweza kudumishwa kuendelezwa, kuigwa na kuachwa. Kutokana na hili yale yanayojitokeza katika ngoma ya n’domo na bakuli nayo lazima kila mdau ayachuje na kuyachukua yanayofaa na kuyaacha yasiyofaa.

Wamakonde, wanataaluma, taasisi mbalimbali, jamii na taifa kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kupitia utafiti huu na kuyachukua yote yaliyokuwa mazuri na kuachana na yale yote yaliyoonyshwa katika utafiti huu kuwa ni udhaifu wa ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde.

5.3       Maapendekezo
Kwa vile ngoma ni kipengele muhimu katika kuendeleza utamaduni wa wamakonde utafiti huu unatoa mapendekezo yafuatayo:-
·         Ngoma za asili zichezwe wakati wa mchana ili kuepuka maovu kama vile uzinifu.
·         Washiriki wa ngoma wajiepusha na kujihusisha na ulevi na matumizi wa dawa za kulevya.
·         Ngoma zisichezwe wakati wa kazi, masomo au wakati wa ibada.
·         Serikali itoe monisha kwa vikundi vya ngoma
·         Watafiti wengine wajitahidi kufanyia utafiti vipengele vingine ambavyo havikuguswa na utafiti huu.
·         Jamii hasa vijana waache kupupia muziki na kusahau ngoma za asili kwani kufanya hivyo ni kupuuza chako na kutukuza za mwenzako.

MAREJEO
Finke J. (2000) Traditional Music & culture of Kenya Blue  Gecko org, Nairobi

Ghasany, H. (2010), Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru, Zanzibar  na Mapinduzi
            ya Afrabia, Library of Congress, NewYork

I PC. (2005), Maarifa  ya Uislamu darasa la watu wazima Juzuu 5 Jamii ya
            Kiislamu, Islamic Propagation  Centre Dar es Salaam

Khamisi ,A .M & Madumla , J.S(1989), Fasihi simulizi katika  Mulika 21. Chuo
                  kikuuu huria Dar es Salaam.

Magwela, D.H. (2008), Uraia shule za msingi 5 kitabu cha mwanafunzi, Oxford
                  University Press (T) Ltd, Dar es Salaam

Masatu, B. (1997), Themes in civics for secondary schools, Book one, NewText
                              book centre Ltd, Dar es Salaam.
Mbonde, J.P. (1993), Wamakonde, Ndanda Mission, Mtwara.

Mbunda, A.A et (1983) Juhudi za kuikomboa nchi yetu, Eastern Africa
                  Publication Limited, Dar es Salaam.

Mosha , I. (2010), Uraia Darasa 6 Kitabu cha mwanafunzi, Ben and company
                  Ltd, Dar es Salaam

Mhando, P & Balisidya,  M. (1976) Fasishi na sanaa za maonyesho, T.P.H.D,
                  Dar es Salaam

Munisi, S.A. (2011) Uraia darasa la 7, Educational, Books Publishers  LTD,
                  Dar es salaam

                    

Ndosi, N.K (2008), Historia darasa 4, Educataional Books publishers LTD,
                  Dar es Salaam.

Omari, C.K. (1981), Urithi wa utamaduni wetu, Tanzania Publishing House,
                  Dar es Salaam

Taasisi ya Elimu Tanzania (1998), maarifa  ya Jamii kitabu cha mwanafunzi
       darasa la 6, E & D Limited, Dar es Salaam

                                                                                                                                 KIAMBATANISHO 1

DODOSO HILI LIJAZWE NA MWENYE UMRI WA MIAKA 39-40 NA AWE NI                                      MMAKONDE WA WILAYA YA NEWALA MKOANI MTWARA

MADA YA UTAFITI: Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli  kwa Utamaduni wa                            Wamakonde
MSIMAMIZI WA UJAZAJI: …………………………….……………………….
TAREHE…………………………………………………………………………….

NAOMBA UJIBU MASWALI YAFUATAYO KAMA MAELEZO YANAVYOKUTAKA.

Andika NDIYO panapoonyesha usahihi na HAPANA pasipoonyesha usahihi.
1.      Wamakonde wanaishi katika Wilaya ya Newala
2.      Umewahi kuona au kucheza ngoma ya n’domo au bakuli
3.      Ngoma zilizotajwa hapo juu bado zinachezwa katika eneo lenu
4.      Vijana kuanzi umri wa mika 15 – 39 wanashiriki katika uchezaji

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI KUTEGEMEANA NA ULIVYOULIZWA
5.      Taja faida tatu (3) za ngoma ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa wamakonde
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………

6.      Unafikiri kwanini vijana wa siku hizi hawapendi kucheza ngoma za asili?
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………
7.         Madhara ya kushiriki katika ngoma ya n’domo na bakuli ni pamoja na
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………
JINA LA MJAZAJI DODOSO ………………………………………………………….
NAMBA YA SIMU …………………………………………. (si lazima)
KAZI …………… MKOA…………. WILAYA…………. UMRI……………………
TARAFA………………….. KATA …………………….. KIJIJI …………………….


JINSIA ME              KE                      KIWANGO  CHA  ELIMU


NAKUSHUKURU  KWA  MSAADA WAKO


KIAMBATANISHO 2

DODOSO HILI LIJAZWE NA MWENYE UMRI WA MIAKA 40 - 80 NA AWE NI                                      MMAKONDE WA WILAYA YA NEWALA MKOANI MTWARA

MADA YA UTAFITI: Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli  kwa Utamaduni wa                            Wamakonde
MSIMAMIZI WA UJAZAJI: …………………………….……………………….
TAREHE…………………………………………………………………………….

NAOMBA UJIBU  MASWALI YAFUATAYO KAMA MAELEZO YANAVYOKUTAKA.

Andika NDIYO panapoonyesha usahihi na HAPANA pasipoonyesha usahihi.
1.      Wamakonde wanaishi katika Wilaya ya Newala
2.      Umewahi kuona au kucheza ngoma ya n’domo au bakuli
3.      Ngoma zilizotajwa hapo juu bado zinachezwa katika eneo lenu
4.      Vijana hatupendi kucheza ngoma ya n’domo na bakuli

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI KUTEGEMEANA NA ULIVYOULIZWA
5.      Faida tatu (3) za ngoma ya n’domo na bakuli ni pamoja na:-
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………

6.      Sababu za vijana kutopenda ngoma ya n’domo na bakuli ni pamoja na:-
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………
7.         Miongoni mwa madhara ya kushiriki katika ngoma ya n’domo na bakuli ni pamoja na
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………
8.         Mambo matatu ambayo yanaweza kuborsha na kuendeleza ngoma ya n’domo ni pamoja na:-        
(a).       …………………………………………………………………………….
(b).       …………………………………………………………………………….
(c).       ……………………………………………………………………………

JINA LA MJAZAJI DODOSO ………………………………………………………….
NAMBA YA SIMU …………………………………………. (si lazima)
KAZI ……………………… MKOA…………………. WILAYA…………………….

JINSIA ME          KE          KIWANGO  CHA  ELIMU


NAKUSHUKURU KWA MSAADA WAKO
           

KIAMBATANISHO 3

HOJAJI  KWA WAZEE WASIOJUA  KUSOMA  NA KUANDIKA

MADA:- Athari za Ngoma ya N’domo na Bakuli  kwa Utamaduni wa  Wamakonde

Mtafiti ………………………………………………            Tarehe………………..
·         Tunaomba utueleze kwa kifupi jina lako, umri wako, kiwango chako cha elimu na kazi yako.
·         Tunadhamilia kuchunguza athari za ngoma  ya n’domo na bakuli kwa utamaduni wa Wamakonde. Tunanaomba ushirikiane nasi kutupatia taarifa zifuatazo:-
1.      Ngoma ya n’domo na bakuli zina mchango gani kwa utamaduni wa wamakonde?
2.      Ngoma ya n’domo na bakuli zina madhara gani kwa utamaduni wa wamakonde?.
3.      Ni nyimbo gani zinazoimbwa wakati wa kucheza ngoma ya n’domo ?
4.      Ni nyimbo gani zinazoimbwa wakati wa kucheza ngoma ya bakuli?
5.      Ni  mambo gani yanayopelekea vijana wasipende kucheza ngoma ya n’domo na bakuli?
6.      Ni mambo gani yafanyike ili kuboresha ngoma ya n’domo na bakuli

Xxxxxxxxxxx Tunakushukuru kwa ushirikiano wako xxxxxxxxxxxxxxx


                                                        


KIAMBATANISHO 4

                                                NYIMBO ZA NGOMA YA N’DOMO

1.      Kunkoma kwa nangalolo waislamu wamekula nditi x2
Kiitikio: Pombe haramu ee

2.      Bakulii  ee  bakulii  ee x2
Kiitikio: Ukanaandike  bakuli kulandana

3.      Ayu mwene  ing’ole  nnani oo mm x2
             Kiitikio: Ayu nangolo oo.

4.      Chiwowawowa woo x2
             Kiitikio: Tulambilana nkanya.

       5.Mchawi kuroga litinji nannuku nwaliya x2
            Kiitikio: Nannuku nwalia ee.

       6.Chii chii chinanganga avetu vahwena x2
              Kiitikio : Chii chinanganga.

                       KIAMBATANISHO 5
  NYIMBO ZA NGOMA YA N’DOMO

1.         Chivamando kuvipedo  ee oo x2
Kiitikio: Chivamando kuvipedo.
2.         Ndoondoo mwinama x2
Kiitikio: oo mwinamaa.
3.         Naliyela oo x2
            Oo Liyele
4.         Serikali ya namwaka kulipembedya x2
            Oo Kulipembedya