Wednesday, July 20, 2011

FAIDA YA MAJI YA ZAMDA

Maji haya yanafaida kubwa kwa KUTIBU aina zote za maumivu ya tumbo.

                      MATUMIZI
kunywa maji ya zamda kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu kwa muda wa siku saba hadi ishirini na moja.INSHAALLAH UTAPONA.

TIBA YA JINO

Mwenye kuhisi maumivu ya jino apate asali vijiko 5 na mdalasini kijiko  kimoja. Mchanganyiko huu utakuwa unapaka kwa nje usawa wa jino linalouma kutwa mara tatu.INSHAALLAH UTAPONA.

TIBA YA MAFUA

(1)Maji ya moto kikombe kimoja cha chai
(2)Asali kijiko kimoja cha chakula
(3)Unga wa mdalasini kijiko kimoja cha chakula

        MATUMIZI
Changanya pamoja halafu uwe unakunywa kutwa mara tatu. kila unapotaka kunywa utakuwa unachanganya wakati huohuo. Tumia dozi hii kwa muda wa siku saba hadi siku kumi na moja.Tiba hii hutibu hata mafua mazito(chronic) na yenye kuziba pua.INSHAALLAH UTAPONA

Saturday, July 16, 2011

TIBA YA KIFUA NA PUMU

Kama  unatatizo  la  kifua  au  pumu  unaweza  kujitibu  kwa  kutumia  dawa  zifuatazo:-

(1) Vijiko vitano  vya unga  wa rifaj
(2) Vijiko  vitano  vya  unga  wa  karafuu
(3) Vijiko  vitano  vya  unga  wa  mjafar
(4) Vijiko  vitano  vya  unga  wa  tangawizi
(5) Vijiko  vitano  vya  unga  wa  alqusus na
(6) Asali mbichi na safi lita  moja

                              NAMNA  YA  KUANDAA
Changanya  vyote  kwa  pamoja  halafu  ukoroge  kwa  muda  mrefu  mpaka  uhakikishe   imechanganyika  vizuri.

                              MATUMIZI
Kula  kijiko kimoja  cha  chakula asubuhi,  mchana  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  kumi  na  moja  hadi  siku  ishirini  na  moja.  INSHAALLAH  UTAPONA

DAWA YA SAHANYOZA

Hii  ni  dawa  ya  kupaka  ambayo  kwa  uwezo  wake  Allah (S.W) INAUWEZO  WA  KUTIBU  MARADHI  MBALIMBALI KAMA  VILE:-

(1) Maumivu  ya  kichwa
(2) Maumivu  ya  mgongo
(3) Maumivu  ya  kiuno
(4) Maumivu  ya mikono
(5) Maumivu  ya miguu
(6) maumivu  ya  viungo
(7) Vidonda  vya  koo
(8) Kung'atwa  na mdudu  na
(9) Fangasi za nje  ya  mwili

DAWA HII NI MCHANGANYIKO  WA DAWA MBALIMBALI  KAMA  VILE; HALIMIT, ELKZAMDA, HABAT SAUDA, ZAITUN. N.K.

MATUMIZI; PAKA SEHEMU  YENYE  MAUMIVU  MARAMBILI  KWA  SIKU  yaani  ASUBUHI  NA  JIONI.

Saturday, July 2, 2011

FAIDIKA NA MAFUTA YA ZAITUNI.


               BISMILLAH  ARRAHMAN  ARRAHIIM      
                       NUFAIKA  NA  MAFUTA  YA  ZAITUNI

Anasema  Allah  (S.W)  KUHUSU  MAFUTA  YA  ZAITUNI:
“…….TUNGI  LILE  NI  KAMA NYOTA  INAYOMEREMETA, INAYOWASHWA KWA  MAFUTA  YANAYOTOKA  KATIKA  MTI  ULIOBARIKIWA  WA  MZAITUNI.  SI  WA  MASHARIKI  WALA  MAGHARIBI.  YANAKARIBIA  MAFUTA  YAKE  KUNG’AA  YENYEWE  INGAWA  MOTO  HAUJAYAGUSA-NURU  JUU  YA  NURU……”(QUR’AN 24:35)

      Mafuta  ya  zaituni  yana  manufaa  mengi  katika  mwili na maisha  ya  binadamu  kwa  ujumla  kama  ifuatavyo;

(1)Mafuta  ya  zaituni  hutibu  maumivu  ya  tumbo  kwa  kunywa  kijiko  1  mara  2 kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  7  hadi  siku 11  inshaallah.

(2)Mafuta  ya  zaituni  hutibu  masheitani  kwa  kusomea  kisomo  cha Ruqia,  mgonjwa  atajipaka  mwili  mzima  mara  moja  kwa  siku  pamoja  na  kutafuna  vitunguu  saumu  punje tatu  wakati wa  kulala  kwa  muda  wa  siku  arobaini  inshaallah.

(3)Mafuta  ya  zaituni ni kinga  ya  masheitani  wa  kijini  na  wa  kibinadamu  kwa  kujipaka  mwili  mzima  mara  moja  kwa  siku.

(4)Mafuta  ya  zaituni  hutibu  ugonjwa  wa  mafua  kwa  kupaka  kwenye  mwamba  wa  pua  na  ndani  ya  matundu  ya  pua  mara  tatu  kwa   siku.

(5)Tiba  ya  vidonda  vya  tumbo; Matumizi  ni  kutia  vijiko  2  vya  chakula  katika  uji    mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  90.

(6) Mafuta  ya  zaituni  hutumika  kama  huduma  ya  kwanza  kwa  aliyekunywa  sumu  kwa  kunywa,  na kwa mwenye  ganzi  au kiharusi hutumia  kwa  kuchua  asubuhi  na  jioni.

(7) Mafuta  ya  zaituni  hutumika katika  kuua  wadudu  wabaya  walioko  tumboni  kwanjia  ya kunywa  kijiko  kimoja mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  saba.

(8) Mafuta  ya  zaituni huongeza  nguvu  za  kiume  kwa kunywa  kijiko  kimoja  kwa  siku  pamoja  na kuuchua  uume  mafuta  yaliyochanganywa  na vitunguu swaumu  kwa  muda  wa  siku  saba  hadi  kumi  na  moja.

(9) Tiba ya ugonjwa  wa  kusahau: paka katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha  chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi  siku 11.

(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi  siku 21.

(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa  muda  wa siku 7 hadi  siku 21.

 Kwa maelezo, ushauri na msada wasiliana na:  Mwalimu NAHONYO,
                        Muslim university of Morogoro
                           P.O.BOX 1031
      fakihimshamu@yahoo.comNahonyo.blogspot.com. 0712829903 or 0784950236