Wednesday, August 31, 2011

TUZINGATIE MAFUNZO YA MWEZI WA RAMADHANI Ndugu zangu wote mnaofuatilia blog yangu, natambua kuwa kuna waislamu na wasio waislamu lakini pamoja na utofauti wetu wa imani bado mafunzo ya Ramadhan yanatugusa wote. Ukarimu, upendo, umoja na mshikamano, kuhurumiana, kusaidiana, kuvumiliana, kuheshimiana pamoja na kufanya matendo mengine ya kiuchamungu ni baadhi ya mafunzo ya mwezi wa Ramadhan. Mwenyezi Mungu yupo wakati wote, halali wala hasinzii, haendi likizo wala hasafiri kwanini tusiendeleze mafunzo ya mwezi mtukufu? Hakuna mwenye uhakika lini ataondoka hapa duniani, unaweza kumuasi mola wako leo, kesho kabla hujatubia ukaondoka duniani, je! Utakuwa mgeni wa nani?aofuatilia blog yangu, natambua kuwa kuna waislamu na wasio waislamu lakini pamoja na utofauti wetu wa imani bado mafunzo ya Ramadhan yanatugusa wote. Ukarimu, upendo, umoja na mshikamano, kuhurumiana, kusaidiana, kuvumiliana, kuheshimiana pamoja na kufanya matendo mengine ya kiuchamungu ni baadhi ya mafunzo ya mwezi wa Ramadhan. Mwenyezi Mungu yupo wakati wote, halali wala hasinzii, haendi likizo wala hasafiri kwanini tusiendeleze mafunzo ya mwezi mtukufu? Hakuna mwenye uhakika lini ataondoka hapa duniani, unaweza kumuasi mola wako leo, kesho kabla hujatubia ukaondoka duniani, je! Utakuwa mgeni wa nani?