Thursday, November 17, 2011

KILA MUISLAMU ANADHIMA YA KUENDELEZA UISALAMU.

Shukrani  zilizo takasika ni zake Allah (s.w.t) asiyekuwa na mshirika katika  Ibada yake  wala katika  ufalme  wake.
Rehema na Amani zishuke juu ya Mtume Muhammad (s.a.w) na wale wote wenye kushikamana naye.
Mwenyezi Mungu ametujaalia wanadamu kuwa makundi mbali mbali  kama vile  masikini  na  matajiri, wafanyakazi  na  wakulima  na  makundi  mengine  mengi. Pamoja na  kuwepo na  makundi  mbali mbali  kila  kundi  linatakiwa  kumcha  Allah (s.w.t) na kuwa mstari wa  mbele  katika  kuendeleza  dini.
Wewe na mimi  tumetamka shahada mbili  na tumekiri katika nyoyo zetu kuwa mwenye jina la Allah ndiye  Mungu wa  kweli  na Muhammad ni Mtume wake, Kukiri na kutamka shahada ni dalili tu ya kujulisha  kuwa sisi ni waislamu. Ili uislamu wetu uweze kukamilika  tunatakiwa  kuyafanya  yale ambayo wametuagiza Allah (s.w.t.) na Mtume wake (s.a.w) na kuyaacha yale ambayo wametukakaza.
Katika  makundi tuliyonayo wanadamu,  kundi la wafanya kazi huwa wamepitia  hatua mbalimbali kama vile shule ya msingi, sekondari, chuoni na  hatimaye kazini. Sasa ewe uliyejaaliwa kuajiriwa ujiulize  ukiwa shule  ya  msingi, sekondari na chuoni, mlianza wangapi, mlifaulu  wangapi na mpaka hivi sasa ni wangapi mnaendelea na kazi?
Je, wale ambao hawakufanikiwa katika yale maeneo ambayo wewe umefanikiwa unafikiri ni uzembe wao  au Allah hakuwawezesha? Na wewe uliyefanikiwa unafikiri umefanikiwa kwa ujanja wako au Allah ndiye aliyekuwezesha?
Allah (s.w.t) humpa amtakaye na humnyima amtakaye, umekuwa miongoni mwa waliopewa na Allah basi nawe utoe katika njia ya Allah ili kuendeleza dini yake si kwaajili ya kumnufaisha mwenyezi mungu bali ni kwaajili ya kutaka radhi ili aendelee kukuruzuku na kulinda  mali  yako.
Mwenyezi Mungu anatuhimiza kwa kusema ndani ya Quran: ENYI MLIOAMINI TOENI KATIKA VILE TULIVYOKUPENI KABLA HAIJAFIKA SIKU AMBAYO HAPATAKUWA (NA) KUJIKOMBOA WALA URAFIKI (WA KUSAIDIANA) WALA UOMBEZI, NA WALIOKUFURU NDIO WALIO JIDHULUMU (KWELIKWELI) Q:2:254.    
Allah (s.w.t.) ametuumba wanadamu akatupa uwezo kuliko viumbe wote, ametupa elimu, akatupa pia uhuru wa kuweza kupanga na kupangua,  kutanda na  kutandua, kufunga  na kufungua  na mengine  mengi.  Tujiulize  enyi wenzangu, katika kipato  chetu  tunatumia kiasi  gani  katika  mambo  ya anasa?
Kwanini tunakunja mikono yetu katika upande wa kundeleza dini yetu?
Sisi tuliojaaliwa kuwa na uhakika wa kipato  tena kwa muda maalumu tunakuwa wazito kutoa. Je, wale wasio kuwa na uhakika wa kipato kwa muda maalumu wataweza? Waislamu wenyewe tusipo iendeleza dini yetu asiye kuwa Muislamu ataweza kuundeleza Uislamu?
Allah (s.w.t) amemsifu binaadamu kwa kusema “ HAKIKA TUMEMUUMBA MWANAADAMU KATIKA UMBO LILILO BORA KABISA”Q 95:4. Hapa inamaana wewe na mimi tumejaliwa  vipawa  vinavyoweza kutuwezesha kutambua dhima ya kuumbwa kwetu na hatima ya maisha yetu hapa duniani na kesho akhera.
Enyi ndugu zangu katika imani na dinI  tujitahidi kutoa bila kuwa na mashaka ya kulipwa katika vile tunavyovitoa, Allah  ameahidi kumlipa kila  mtu kwa kila akifanyacho kiwe cha  kheri au shari, kidogo au kikubwa, akiwa ametoa kwa siri au wazi kama  anavyosema ndani ya Quran 2:274 “WALE WANAOTOA MALI  ZAO USIKU NA MCHANA KWA SIRI NA DHAHIRI, WANAUJIRA WAO KWA MOLA WAO, WALA HAITAKUWA KHOFU JUU YAO  WALA HAWATAHUZUNIKA”
Ewe Mwenyezi Mungu , kila atakaye kunjua  mkono wake na kutoa kwako basi mtengenezee mambo yake hapa Duniani na Kesho Akhera.

KILA MUISLAMU ANDHIMA YA KUENDELEZA UISALAMU.

Shukrani  zilizo takasika ni zake Allah (s.w.t) asiyekuwa na mshirika katika  Ibada yake  wala katika  ufalme  wake.
Rehema na Amani zishuke juu ya Mtume Muhammad (s.a.w) na wale wote wenye kushikamana naye.
Mwenyezi Mungu ametujaalia wanadamu kuwa makundi mbali mbali  kama vile  masikini  na  matajiri, wafanya  kazi  na  wakulima  na  makundi  mengine  mengi. Pamoja na  kuwepo na  makundi  mbali  mbali  kila  kundi  linatakiwa  kumcha  Allah (s.w.t) na kuwa msari wa  mbele  katika  kuendeleza  dini.
Wewe na mimi  tumetamka shahada mbili  na tumekirir katika nyoyo zetu kuwa mwenye jina la Allah ndiye  mungu wa  kweli  na Muhammad ni Mtume wake, kukiri na kutamka shahada ni dalili tu ya kujulisha  kuwa sisi ni waislamu. Ili uislamu wetu uweze kukamilika  tunatakiwa  kuyafanya  yale ametuagiza Allah (s.w.t.) na Mtume wake na kuyaacha yale ambayo wametukakaza.
Katika  makundi tuliyonayo wanadamu  kundi la wafanya  kazi huwa wamepitia  hatua mbali  mbali kama vile shule ya msingi, sekondari, chuoni na  hatimaye kazini. Sasa ewe uliye jaaliwa muajiriwa ujiulize  ukiwa shule  ya  msingi, sekondari na chuoni, mlianza wangapi, mlifaulu  wangapi na mpaka hivi sasa ni wa ngapi mnaendelea na kazi?
Je wale ambao hawaku fanikiwa katika yale maeneo ambayo wewe umefanikiwa unafikiri ni uzembe wao  au Allah hakuwawezesha? Na wew uliye fanikiwa unafikiri umefanikiwa kwa ujanja wako au Allah ndiye aliyekuwezesha?
Allah (s.w.t) humpa amtakaye na humnyima amtakaye, umekuwa miongoni mwa waliopewa na Allah basi nawe utowe katika njia ya Allah ili kuendeleza dini yake si kwaajili ya kumnufaisha mwenyezi mungu bali ni kwaajili ya kutaka radhi ili aendelee kukuruzuku na kulinda  mali  yako.
Mwenyezi Mungu anatuhimiza kwa kusema ndani ya Quran: ENYI MLIOAMINI TOENI KATIKA VILE TULIVYOKUPENI KABLA HAIJA FIKA SIKU AMBAYO HAPATAKUWA (NA) WALA URAFIKI (WA KUSAIDIANA) WALA UOMBEZI, NA WALIOKUFURU NDIO WALIO JIDHULUMU (KWELIKWELI) Q:2:254.    
Allah (s.w.t.) ametuambia wanadamu atatupa uwezo kuliko viumbe wote, ametupa elimu, akatupa pia uhuru wa kuweza kupanga na kupangua,  kutanda na  kutandua, kufunga  na kufungua  na mengine  mengi.  Tujiulize  enyi wenzangu, katika kipato  chetu  tunatumia kiasi  gani  katika  mabo  ya anasa?
Kwanini tunakunja mikono yetu katika upnde wa kundeleza dini yetu?
Sisi tuliojaaliwa kuwa na uhakika wa kupata tena kwa muda maalumu tunakuwa wazito wakutoa je, wale wasio kuwa na uhakika wa kipato kwa muda maalumu wataweza? Waislamu wenyewe tusipo iendeleza dini yetu asiye kuwa Muislamu ataweza kuundeleza Uislamu?
Allah (s.w.t) amemsifu binaadamu kwa kusema “ HAKIKA TUMEMUUMBA MWANAADAMU KATIKA UMBO LILILO BORA KABISA” 95:4. Hapa inamaana wewe na mimi tumejaliwa  vipawa  vinavyoweza kutuwezesha kutambua dhima ya kuumbwa kwetu na hatima ya maisha yetu hapa duniani na kesho akhera.
Enyi ndugu zangu katika imani na din tujitahidi kutoa bila kuwa na mashaka ya kulipwa katika vile tunavyovitoa, Allah  ameahidi kumlipa lika mtu kwa kila akifanyacho kiwe ch kheri au shari, kidogo au kikubwa, akiwa ametoa kwa siri au wazi kama navyo sema ndani ya Quran 2:274 “WALE WANAOTOA MALI ZAO USIKU NA MCHANA KWASIRI NA DHAHIRI, WANAUJIRA WAO KWA MOLA WAO, WALA HAITAKUWA KHOFU JUU YAO  WALA H WATA HUZUNIKA”
Ewe Mwenyezi Mungu , kila atakaye kunjua  mkono wake na kutoa kwako basi mtengenezee mambo yake hapa Duniani na Kesho Akhera.

SALAMU ZA NDOA SEHEMU YA (II)

Kila sifa njema ni  zake Allah (s.w.t) muumba wa viumbe wote. Rehema za mwenyezi Mungu zishuke kwa Mtume Muhammadi (s.a.w) na watu wake wote.
TALAKA ni halali lakini ni halali inayochukiza kwa mwenyezi Mungu kwa sababu ya maudhi na madhara yanayo patikana baada ya wanandoa kutengana. Juu ya hii Mtume (s.a.w) anasema “ JAMBO  LA HALALI KULIFANYA LAKINI LINACHUKIZA SANA MBELE YA MWENYEZI MUNGU (S.W.T) NI MTU KUTOA TALAKA (Yaani kumuacha mke)”
Watu wanapokuwa katika ndoa wajue kuwa wako katika vazi, rehema, upendo na amani, lakini wanapoachana mambo hayo yote hutoweka na kusababisha matatizo na maudhi na pengine hujiingiza katika  maovu, na kama walibahatika kupata watoto basi watakosa malezi ya wazazi wote kwa pamoja na hivyo kuwafanya wakose kujengewa msingi mzuri wa KIMAADILI.
Katika uislamu hatuna mafunzo yanayo wafanya watu watengane, bali mafunzo tuliyonayo ni yakuwasuluhisha watu wapatane, na jambo hili ni jukumu la kila aliye kiongozi kuhakikisha kuwa anawapatanisha watu  waliogombana. Mwanamke anaweza kupewa talaka kama atafanya makosa makubwa yaliyowazi, kuwa muasi katika dini au kwa sababu yeyote ya msingi ya kisheria. Lakini hatua hii iwe ni hatua ya mwisho baada ya kutanguliwa na hatua zingine za awali za upatanishi.
Waliowengi miongoni mwetu wanafikiri kuwa talaka ni lazima tu iandikwe kwenye karatasi. Talaka inaweza kuandikwa, katika karatasi au inaweza kutolewa kwa matamko tu kama vile, nimekuacha, uko huru, ondoka tu , si mke wangu n.k. itaswihi maadamu tu yametolewa maneno hayo kwa nia ya talaka.    
Talaka inawahusu wale walio funga ndoa kisheria. Ifahamike kuwa mtu asiandike au kuzungumza jambo la talaka akasema ati nilikiwa ninatania, utani wake hautakubaliwa kisheria.
Mume anaruhusiwa kumiliki talaka tatu (3) lakini cha ajabu ni kwamba utamuona mtu anamtolea mkewe talaka zaidi ya tatu (3) huo sio uislamu bali ni USHETANI. Na hairuhusiwi kuzitoa talaka kwa  pamoja, bali talaka hutolewa moja moja. Na talaka ya kwanza na yapili huitwa talaka REJEA, yaani mume anaruhusiwa kumjerea mke wake ndani ya EDA yake. Na kama EDA yake ikiisha hana ruhusa kumrejea bali kwa ndoa nyengine tena akitaka. Na talaka ya tatu inaitwa talaka ya BAYANA, na mwenye kumpa mke talaka tatu hana ruhusa ya kumrejea mpaka aolewe na mume mwingine na sheria hapa inasema mpaka afanye naye tendo la ndoa halafu amuache kisha akae EDA amalize ndipo atapata ruhusa ya kumuoa tena kama anataka.
EDA zimegawanyika namna mbili yaani eda ya mwanamke kufiwa na mumewe na EDA ya talaka. EDA ya mwanamke aliyefiwa na mume wake kama ni mjamzito basi EDA itaisha mara atakapojifungua na kama si mjamzito atakaa  kwa muda wa miezi minne (4) na siku kumi (10) na mwanamke mwenye kukaa EDA kwa ajili ya kupewa talaka  kama ni mjamzito naye EDA yake itaisha mara tu baada ya kujifungua  na kama hana ujauzito basi atakaa kwa muda wa miezi mitatu. Mwanamke aliyepewa talaka moja  ndiye anayezungumziwa hapa.
Mwanamke mwenye kukaa EDA asitolewe hapo katika nyumba na wala hana ruhusa ya kutoka mwenyewe isipokuwa  akileta mambo ya ouvu yaliyo wazi inaruhusiwa kumfukuza. Mke anapokaa EDA basi ni jukumu la mume kumpa huduma huyo mke aliyempa talaka, vilevile ni jukumu la jamaa wa mume kumhudumia  mke aliyefiwa na mume wake mpaka EDA itakapoisha.
Huduma inayozungumziwa hapa ni ile ya mahitaji ya msingi na wala siyo kufanya naye ZINAA.
Ama watu wengi wanauliza ati, kwa nini mke akae EDA na mume asikae EDA? Kwa kifupi ni kwamba mume ndiye mchunga wa mke kwa hiyo muda wa mke ambao anakaa EDA ni kumpa nafasi ajiangalie hali yake kama  anaujauzito au la vilevile kwa upande wa EDA ya talaka inakuwa ni nafasi ya kuwafanya waliotengana kuombana msamaha na hivyo kufungua ukurasa mpya.
Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba umuongoze kila anayesoma ujumbe huu na umruzuku kila anayesambaza ujumbe huu na vilevile uwape nguvu na moyo waislamu wengine kufanya kazi kama hii angalau kutoa mwongozo au ukumbusho kwa wengine. Mungu akiendelea kuniwezesha kwa hali na mali sitachoka daima nanyi wasomaji naomba mniombee mafanikio katika kazi hii INSHAALAAH.