Saturday, July 4, 2015

NIUNGENI MKONO WANANEWALA WOTE

Namshukuru Mwenyezi Mungu muummba wa mbingu na ardhi na vilivyomo humo na vilivyo baina ya mbingu na ardhi. Ninania ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Newala Vijijini tukijaliwa kupata jimbo na kama vigezo havitakidh i vya kupata jimbo basi inshaallah nitagombea jimbo la Newala natarajia kupitia Chama cha Mapinduzi.

Ombi langu kubwa kwenu wadau wa blog hii  na WanaNewala mniunge mkono kwania yangu hii. Naingia nikiwa najua kuwa ninadhima kubwa ya kurudisha matumaini kwa wanainchi waliokosa imani kwa chama cha mapinduzi na serikali yake, vilevile najua kuwa kuna makundi hayajaguswa kabisa.

Ninania  ya dhati kabisa naomba mniunge mkono kwa hali na mali ,  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili Wananewala inshaallah. Changamoto  za Newala wala hazihitaji elimu ya chuo kikuu kuweza kuzibaini au kuzitatua bali zinahitaji umoja, mshikamano na uongozi madhubuti chini ya Fakihi Mshamu kama Mbunge mtarajiwa wa Jimbo jipya la\ Newala.

Wadau wenzangu wa Newala, kumbukeni  kuwa mageuzi ya aina yeyote yanahitaji  mambo makuu mawili; wakati  na umoja. Ni matumaini yangu kuwa wakati umekwishafika kilichobaki ni ninyi kuungana nami na kuunda umoja ili tulete mageuzi. Nakuja kwenu nikijua kuwa HAYA TULIYONAYO NDIO MAISHA YENYEWE NA HAKUNA MAISHA MENGINE ZAIDI YA HAYA TULIYONAYO KWA HAPA  DUNIANI NA KILA AHADI NI  YENYE  KUULIZWA  MBELE  YA MWENYEZI MUNGU.

Tunayo  mengi yenye tija kwa  ustawi wa Wananewala, wakati ukifika tutawaelezeni  na tutawaomba mtuunge mkono. WITO WANGU  KWENU NI KUWA MAKINI  NA  WAGOMBEA  WATAKAOJARIBU  KUZINUNUA AKILI  ZENU ILI MSIFANYE CHAGUO  SAHIHI, KUMBUKENI KUWA MIAKA MITANO NI MINGI SANA ENDAPO MTAKUWA KATIKA SHIDA  NA  M ANUNG'UNIKO  NA NI MICHACHE ENDAPO MTAKUWA KATIKA FARAJA NA FURAHA, AKILI YAKO  NDIO  DHAMANA  YAKO.

Friday, June 12, 2015

TUJIHADHARI NA WAGOMBEA WATOA RUSHWA



Kila sifa njema ni zake  Mwenyezi Mungu aliyemuumba Mwanadamu  katika umbo bora. Watanzania wenzangu, uchaguzi unapokaribia, wagombea huonekana wapole, wakarimu, wenye kauli zenye matumaini na wenye kuwajali wananchi. Kabla na baada ya uchaguzi ukali, majivuno, dharau na ubabe kwa wananchi huwa ndio kawaida yao.
Leo si ajabu kuwaona wagombea wakigawa fedha, nguo na vitu vingine bila hata kuombwa. Tunawapongeza kwa moyo wao wa kutoa lakini wanatakiwa watupe majibu kwa nini misaada yao ije wakati huu wa uchaguzi na si kabla ya hapo? Vitu hivi ni nini kama si RUSHWA? Watanzania wenzangu, hivi tuko tayari kuuza ukristo na uislamu wetu? Dini zetu zinatuonya juu ya kutoa na kupokea RUSHWA. Uislamu, mtume Muhammadi (S.a. w) anasema “Mwenyezimungu amemlaani mtoa Rushwa,mpokea Rushwa na anayewaunganisha wawili hawa”. Katika Qur’ani Mwenyezimungu anasema”NA UTAWAONA WENGI KATIKA WAO WANAKIMBILIA KATIKA DHAMBI NA UADUI NA ULAJI WAO WA HARAMU. BILA SHAKA WAYAFANYAYO HAYO NI MABAYA KABISA (Q 5:62)” Ndani ya Bibilia nako wakristo wamekemewa vibaya”. KWELI JEURI HUMPUMBAZA MWENYE HEKIMA, NA RUSHWA HUHARIBU UFAHAMU (MHUBIRI:7:7).
Watanzania wenzangu RUSHWA ni kipimo cha kumtambua kiongozi bora na asiyebora. Kama mgombea akikujia kukuomba kura yako na kukupa kitu kidogo ujue wazi kuwa huyo amepoteza sifa ya kuwa kiongozi, ukimchagua kiongozi kwa sababu tu ametoa RUSHWA ujue kuwa ni kumpa meno yatakayo mjengea dharau na majivuno juu yako. Akichaguliwa kwa njia ya RUSHWA kiongozi hujiona pesa zake ndizo zilizomchagua na si wewe mtanzania mwenzangu uliyempigia kura.
Leo ukitangaza nia ya kugombea nafasi fulani watu watakuuliza “unapesa?”. Tabia hii ndiyo inayopelekea tupate viongozi wabovu ati kwa sababu tu wanapesa, asiyekuwa na pesa hata kama anasifa njema  watu hawamjali. Naikumbusha nafsi yangu na yako ewe uliyejaliwa akili timamu, RUSHWA ni adui katika jamii, Serikalini na katika dini, tujilazimishe kuikataa ili tusichague PUMBA tukaacha MCHELE.
Poleni watanzania wenzangu mnaodanganyika kwa sasa mkawa tayari  kupokea RUSHWA na kujiingiza katika upofu wa maamuzi. Ombi langu kwenu mchagueni kiongozi bora na si bora kiongozi, hata kama mtu amewajieni kwa baiskeli lakini akawa na hoja thabiti zinazoonesha matumaini mchangueni atawafaeni kuliko huyo mtoa RUSHWA.
FAKIHI S. MSHAMU (MWL NAHONYO).
SIMU: 0784950236/0712829903.
Blog:www.nahonyo.blogspot.com.


MFAHAMU FAKIHI MSHAMU (MWL NAHONYO).


Huyu ni mwalimu kitaaluma. Ni mtoto wa Mzee Salumu Mshamu na Bi Esha Namalove wa Mtongwele Chilangala Wilayani Newala Mkoani Mtwara.
Alizaliwa tarehe 01/05/1980 katika kijiji cha Mtongwele  Chilangala.
1989 – 1995: Alisoma elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mbonde wilaya ya Newala.
1996 – 1999: Alisoma elimu ya sekondari katika shule ya kutwa Mnyambe Wilaya ya Newala .
2003: Alijiunga na chuo cha ualimu Bustani Wilayani Kondoa mkoani Dodoma kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti.
2004: Aliajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kama Mwalimu na alipangiwa shule ya Msingi Mbonde ambako anafundisha hadi leo.
2010: Alifanya mtihani wa kidato cha sita (6) katika shule ya Ndanda kama mwanafunzi wa kujitegemea. Baada ya matokeo alijiunga na chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ambako alihitimu na kutunukiwa shahada ya Ualimu (B.A Education) Mwaka 2013.

Friday, June 5, 2015

MFAHAMU FAKIHI SALUMU MSHAMU (MWL. NAHONYO)

Huyu ni mwalimu kitaaluma aliyefikia chuo kikuu. Huyu ni mtoto wa Mzee Salumu Mshamu na Bi Esha Namalove wa Mtongwele Chilangala wilayani Newala.
Alizaliwa tarehe 01/05/1980 katika kijiji cha Mtongwele Chilangala, mwaka 1989-  1995 alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi Mbonde wilayani Newala.
Mwaka 1996 -  1999 alisoma elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya kutwa Mnyambe wilayani Newala.
Mwaka 2003 alijiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Bustani wilayani Kondoa mkoani Dodoma kwa ngazi ya cheti.
Mwaka 2004 aliajiriwa na Halmashauri ya Wilaya kama mwalimu wa shule ya msingi Mbonde.
Mwaka 2010 alifanya mtihani wa kidato cha sita kama mtahiniwa wa kujitegemea, baada ya matokeo alijiunga na chuo kikuu cha waislam Morogoro kwa ajili ya shahada ya ualimu ambapo mwaka 2013 alihitimu na kutunukiwa shahada.

TUNU ALIYOJALIWA; NGAZI ZOTE ZA UALIMU ALIZOPITIA AMEWAHI KUWA KIONGOZI. MAASHAALLAH