Friday, December 9, 2011

SALAMU ZA NDOA SEHEMU 1

         Shukrani zisizo  na  kikomo  ni  zake Allah, Muumba  na  mlinzi  wa  viumbe  wote. Rehema  na  amani  zishuke  kwake Mtume Muhammad(s.a.w) na watu  wake  wote pamoja  na  maswahaba  wake.

         Ndoa  ni lazima/wajibu kwa mtu ambaye  hawezi  kujizuia  na  ZINAA na  akawa  ni  mwenye  uwezo  juu  ya  MAHARI  na matumizi (mahitaj /huduma)  kwa mke. Katika  ndoa MAHARI ni  kitu  cha lazima  kwa jina  jingine  huitwa  SADAKA, hii  ni mali  anayotoa  mume  kumpa mke  na wala  si  wazazi  au jamaa wa mke  bali  ni  yake  mwenyewe  mwanamke. Lakini  mke  anaweza  kuamua  kwa  hisani  yake  mwenyewe  kuwapa  wazazi  wake  au  kwenda  kutumia  na  mume  wake.  Wazazi  na  jamaa  kupanga  kiasi  cha  MAHARI  na  kutumia  bila  kumshirikisha binti  mwenyewe  ni  makosa  makubwa  ndugu  zangu.

         Makosa  mengine  tunayofanya ni  kutoza  MAHARI  kubwa,  jambo  hili  linapelekea  wanaume  waliowengi  washindwe  kuona  kwasababu  ya  kukosa  uwezo  na  hatimaye  wanaendelea  na  maasi  ya  ZINAA  na  wale  wanaobahatika kuoa  kwa MAHARI  hiyo  kubwa  wanabaki  hata  hawana  kianzio  katika  maisha  yao  ya  ndoa. MAHARI haina kikomo/ mpaka kwa uchache au wingi wake lakini kinacho takiwa MAHARI hiyo iwe na manufaa na thamani , Mtume (S.A;W) juu ya hili anasema "TOENI ANGALAU PETE YA CHUMA"

         Katika kuchumbia ni  SUNNA   kwa  mume kutazama  uso  na  viganja  vya  mchumba  wake na wakati wa kutazama awapo ndungu wa mke, juu la hili mtume anasema "ATAKAPOCHUMBIA MMOJA WENU MWANAMKE AKIWEZA KUYATAZAMA YALE YATAKAYO MPELEKEA KUMUOWA KWAKE BASI AFANYE". Hapa tunaambiwa  kutazama  uso na viganja  vyake  na wala  si  kufanya  nae  ZINAA  ati tunafanya majaribio (practical ) majaribio. kufanya hivyo kabla ya ndoa ni makosa makubwa na hukumu yake ni kuchapa BAKORA MIA (100). kwa Mume na Mke, kwa vile ni wazinifu.
       
       Ndoa ya kiislam ili iswihi /ikubalike ni lazima  awepo Mlezi /Msaidizi na mashahidi wawili waislamu waliowaadilifu, Waliohuru na wawe wanaume (kwa pande zote mbili ). Juu ya hili Mtume  (S.A.W) anasema MASHAIDI WAADILIFU". Sasa je, Ndoa hizo za mkeka hao wote wanakuwepo? kama wanakosekana uhalali unatoka wapi?
     
       Enyi ndugu zangu, ni haramu /haitakiwi kwa muislamu kumuoa au kuolewa na asiye kuwa muislamu na vilevile ni haramu kuolewa au kumuoa ndugu yako kwa ukaribu wa ukoo au KUNYONYA au UKWE au kuwachanganya ndugu pamoja (yaani mkumbwa na mdogo au mapacha kuwaoa wote kwa pamoja kama wafanyavyo wengine).

     Enyi ndugu zangu mliokili upweke na utukufu wa Allah, hivi jinsi tunavyosherekea ndoa zetu ndivyo inavyotakiwa katika ndoa, tunaweka Mikesha ambayo inaambatana na muziki na pengine na pombe. jamani ndiyo ni furaha lakini mnaonaje furaha hiyo tujisherekea kwa kusoma Quran, kupeana mawaidha, kusoma riwaya za Mtume (S.A.W). kuburudika kwa Qaswida na pengine hata kwa Dhiki?.
     
     Kumbuka: "MJNGA NCHI NI MWANANCHI" na "MJENGA DINI NI MWANADINI (MUUMINI)". Kwa hiyo basi tufanye mambo yanayoendeleza dini na wala si yale yanayopunguza thamani ya dini. Ndoa ni jambo la furaha na Kheri kwa hiyo tutumie nafasi hiyo kuomba dua ili Allah alete mafanikio katika ndoa badala ya kuweka kanda za muziki tuweke kanda za dini. tuzinduke zangu ili tufanikiwe hapa Duiniani na kesho Akhera.

     Kwa leo namalizia kwa maneno ya kiongozi watu Mtume (S.A.W) pale aliposema "MTU MWENYE KUWEZA MIONGONI  MWENU KUOA BASI AOE HAKIKA LINASITIRI JICHO NA NI KINGA YA UTUPU NA ASIYEWEZA  (KUOA ) BASI NI JUU YAKE KUFUNGA"
"MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE NDIO WANAOJUA KULIKO MIMI NA WEWE.            
                                     SALAMU HIZI ZIMETOLEWA NAMI MCHACHE WA ELIMU.
                                                                   MWL. NAHONYO  (FASANA)
                    

















NUFAIKA NA MAFUTA YA MISKI

Miski  ni  mama  wa  mafuta yote  mazuri  duniani. Kutokana  na  ubora  au  umuhimu  wake  katika  tiba na  manukato  watu  wengi wamekuwa  wakichakachua  na  kuzalisha  miski  feki.


UNAWEZAJE  KUTAMBUA  MISKI  FEKI  NA  HALISI?
 Unaweza  kutambua  kwa  kunusa,  kupima  uzito  na  ladha. Kwa  upande  wa   ladha,  miski  halisi  inakuwa  na  ladha  ya  uchungu  isiyochanganyika  na  sukari,  na  kama  utaonja  basi  utapata  msisimuko  fulani. Pia  kama  utayasomea Ruqia  na  kumpakaa  mgonjwa  wa  masheitani  athari  zake  huonekana  maramoja.



 MATUMIZI  YA  MAFUTA  YA  MISIKI  KAMA  TIBA 

 1. Ni  kinga  na  tiba  ya  masheitani  wa  kijini  na  kibinadamu.  MATUMIZI; Changanya  mafuta  ya  miski  na  ya  zaituni  halafu  uwe  unajipakaa mwilimzima asubuhi na jioni. ukkosa mafuta ya zaituni unaweza kutumia mafuta ya miski pekeyake.
2.Kusafisha na kufungua milango ya fahamu-MATUMIZI; Nusa marakwamara.

3.Kuongeza hamu ya chakula cha usiku kwa wanandoa. MATUMIZI; weka maji katika glasi halafu dondoshea matone matatu ya miski, halafu unywe na kujipaka sehemu nyeti dakika tano kabla ya kwenda chakulani. hii ni kwa wanaume na wanawake.

4. Kusafisha sehemu nyeti. MATUMIZI; Wanawake baada ya kumaliza siku zao wanaweza kutumia mafuta haya kwa kuondoa harufu, lakini pia kwa kuongeza ashiki (hamu). ONYO: Usitumiye bila kuchanganya na maji na usitumiye kama hauko katika ndoa nakama uko mbalimbali na mume wako.

5. Tiba ya uke ulio legea. MATUMIZI; Changanya na maji halafu uwe unanawa kwa ajili ya kukaza uke, kupunguza maji na kufanya sehemu hiyo kuwa ndogo.

6. Kipimo cha maradhi ya kijini. MATUMIZI; Pakaa matundu thelathini na mbili wakati wa usiku ambayo ni ncha za vidole, chuchu, macho, masikio, pua, mbeleni na nyumani. ukipakaa kama unasumbuliwa na jini basi utaummwa na kichwa au kupata mawengemawenge.

7.Tiba ya fangasi. MATUMIZI; Pakaa sehemu yenye fangasi marambli kwa siku, kwa muda wa siku saba Inshaallah utapona