Friday, December 9, 2011

NUFAIKA NA MAFUTA YA MISKI

Miski  ni  mama  wa  mafuta yote  mazuri  duniani. Kutokana  na  ubora  au  umuhimu  wake  katika  tiba na  manukato  watu  wengi wamekuwa  wakichakachua  na  kuzalisha  miski  feki.


UNAWEZAJE  KUTAMBUA  MISKI  FEKI  NA  HALISI?
 Unaweza  kutambua  kwa  kunusa,  kupima  uzito  na  ladha. Kwa  upande  wa   ladha,  miski  halisi  inakuwa  na  ladha  ya  uchungu  isiyochanganyika  na  sukari,  na  kama  utaonja  basi  utapata  msisimuko  fulani. Pia  kama  utayasomea Ruqia  na  kumpakaa  mgonjwa  wa  masheitani  athari  zake  huonekana  maramoja.



 MATUMIZI  YA  MAFUTA  YA  MISIKI  KAMA  TIBA 

 1. Ni  kinga  na  tiba  ya  masheitani  wa  kijini  na  kibinadamu.  MATUMIZI; Changanya  mafuta  ya  miski  na  ya  zaituni  halafu  uwe  unajipakaa mwilimzima asubuhi na jioni. ukkosa mafuta ya zaituni unaweza kutumia mafuta ya miski pekeyake.
2.Kusafisha na kufungua milango ya fahamu-MATUMIZI; Nusa marakwamara.

3.Kuongeza hamu ya chakula cha usiku kwa wanandoa. MATUMIZI; weka maji katika glasi halafu dondoshea matone matatu ya miski, halafu unywe na kujipaka sehemu nyeti dakika tano kabla ya kwenda chakulani. hii ni kwa wanaume na wanawake.

4. Kusafisha sehemu nyeti. MATUMIZI; Wanawake baada ya kumaliza siku zao wanaweza kutumia mafuta haya kwa kuondoa harufu, lakini pia kwa kuongeza ashiki (hamu). ONYO: Usitumiye bila kuchanganya na maji na usitumiye kama hauko katika ndoa nakama uko mbalimbali na mume wako.

5. Tiba ya uke ulio legea. MATUMIZI; Changanya na maji halafu uwe unanawa kwa ajili ya kukaza uke, kupunguza maji na kufanya sehemu hiyo kuwa ndogo.

6. Kipimo cha maradhi ya kijini. MATUMIZI; Pakaa matundu thelathini na mbili wakati wa usiku ambayo ni ncha za vidole, chuchu, macho, masikio, pua, mbeleni na nyumani. ukipakaa kama unasumbuliwa na jini basi utaummwa na kichwa au kupata mawengemawenge.

7.Tiba ya fangasi. MATUMIZI; Pakaa sehemu yenye fangasi marambli kwa siku, kwa muda wa siku saba Inshaallah utapona

No comments:

Post a Comment