BISMILLAH ARRAHMAN ARRAHIIM
NUFAIKA NA MAFUTA YA ZAITUNI
Anasema Allah (S.W) KUHUSU MAFUTA YA ZAITUNI:
“…….TUNGI LILE NI KAMA NYOTA INAYOMEREMETA, INAYOWASHWA KWA MAFUTA YANAYOTOKA KATIKA MTI ULIOBARIKIWA WA MZAITUNI. SI WA MASHARIKI WALA MAGHARIBI. YANAKARIBIA MAFUTA YAKE KUNG’AA YENYEWE INGAWA MOTO HAUJAYAGUSA-NURU JUU YA NURU……”(QUR’AN 24:35)
Mafuta ya zaituni yana manufaa mengi katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla kama ifuatavyo;
(1)Mafuta ya zaituni hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11 inshaallah.
(2)Mafuta ya zaituni hutibu masheitani kwa kusomea kisomo cha Ruqia, mgonjwa atajipaka mwili mzima mara moja kwa siku pamoja na kutafuna vitunguu saumu punje tatu wakati wa kulala kwa muda wa siku arobaini inshaallah.
(3)Mafuta ya zaituni ni kinga ya masheitani wa kijini na wa kibinadamu kwa kujipaka mwili mzima mara moja kwa siku.
(4)Mafuta ya zaituni hutibu ugonjwa wa mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.
(5)Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.
(6) Mafuta ya zaituni hutumika kama huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au kiharusi hutumia kwa kuchua asubuhi na jioni.
(7) Mafuta ya zaituni hutumika katika kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwanjia ya kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.
(8) Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja.
(9) Tiba ya ugonjwa wa kusahau: paka katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.
(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
Kwa maelezo, ushauri na msada wasiliana na: Mwalimu NAHONYO,
Muslim university of Morogoro
P.O.BOX 1031
fakihimshamu@yahoo.com, Nahonyo.blogspot.com. 0712829903 or 0784950236
No comments:
Post a Comment