Shukrani zilizo takasika ni zake Allah (s.w.t) asiyekuwa na mshirika katika Ibada yake wala katika ufalme wake.
Rehema na Amani zishuke juu ya Mtume Muhammad (s.a.w) na wale wote wenye kushikamana naye.
Mwenyezi Mungu ametujaalia wanadamu kuwa makundi mbali mbali kama vile masikini na matajiri, wafanya kazi na wakulima na makundi mengine mengi. Pamoja na kuwepo na makundi mbali mbali kila kundi linatakiwa kumcha Allah (s.w.t) na kuwa msari wa mbele katika kuendeleza dini.
Wewe na mimi tumetamka shahada mbili na tumekirir katika nyoyo zetu kuwa mwenye jina la Allah ndiye mungu wa kweli na Muhammad ni Mtume wake, kukiri na kutamka shahada ni dalili tu ya kujulisha kuwa sisi ni waislamu. Ili uislamu wetu uweze kukamilika tunatakiwa kuyafanya yale ametuagiza Allah (s.w.t.) na Mtume wake na kuyaacha yale ambayo wametukakaza.
Katika makundi tuliyonayo wanadamu kundi la wafanya kazi huwa wamepitia hatua mbali mbali kama vile shule ya msingi, sekondari, chuoni na hatimaye kazini. Sasa ewe uliye jaaliwa muajiriwa ujiulize ukiwa shule ya msingi, sekondari na chuoni, mlianza wangapi, mlifaulu wangapi na mpaka hivi sasa ni wa ngapi mnaendelea na kazi?
Je wale ambao hawaku fanikiwa katika yale maeneo ambayo wewe umefanikiwa unafikiri ni uzembe wao au Allah hakuwawezesha? Na wew uliye fanikiwa unafikiri umefanikiwa kwa ujanja wako au Allah ndiye aliyekuwezesha?
Allah (s.w.t) humpa amtakaye na humnyima amtakaye, umekuwa miongoni mwa waliopewa na Allah basi nawe utowe katika njia ya Allah ili kuendeleza dini yake si kwaajili ya kumnufaisha mwenyezi mungu bali ni kwaajili ya kutaka radhi ili aendelee kukuruzuku na kulinda mali yako.
Mwenyezi Mungu anatuhimiza kwa kusema ndani ya Quran: ENYI MLIOAMINI TOENI KATIKA VILE TULIVYOKUPENI KABLA HAIJA FIKA SIKU AMBAYO HAPATAKUWA (NA) WALA URAFIKI (WA KUSAIDIANA) WALA UOMBEZI, NA WALIOKUFURU NDIO WALIO JIDHULUMU (KWELIKWELI) Q:2:254.
Allah (s.w.t.) ametuambia wanadamu atatupa uwezo kuliko viumbe wote, ametupa elimu, akatupa pia uhuru wa kuweza kupanga na kupangua, kutanda na kutandua, kufunga na kufungua na mengine mengi. Tujiulize enyi wenzangu, katika kipato chetu tunatumia kiasi gani katika mabo ya anasa?
Kwanini tunakunja mikono yetu katika upnde wa kundeleza dini yetu?
Sisi tuliojaaliwa kuwa na uhakika wa kupata tena kwa muda maalumu tunakuwa wazito wakutoa je, wale wasio kuwa na uhakika wa kipato kwa muda maalumu wataweza? Waislamu wenyewe tusipo iendeleza dini yetu asiye kuwa Muislamu ataweza kuundeleza Uislamu?
Allah (s.w.t) amemsifu binaadamu kwa kusema “ HAKIKA TUMEMUUMBA MWANAADAMU KATIKA UMBO LILILO BORA KABISA” 95:4. Hapa inamaana wewe na mimi tumejaliwa vipawa vinavyoweza kutuwezesha kutambua dhima ya kuumbwa kwetu na hatima ya maisha yetu hapa duniani na kesho akhera.
Enyi ndugu zangu katika imani na din tujitahidi kutoa bila kuwa na mashaka ya kulipwa katika vile tunavyovitoa, Allah ameahidi kumlipa lika mtu kwa kila akifanyacho kiwe ch kheri au shari, kidogo au kikubwa, akiwa ametoa kwa siri au wazi kama navyo sema ndani ya Quran 2:274 “WALE WANAOTOA MALI ZAO USIKU NA MCHANA KWASIRI NA DHAHIRI, WANAUJIRA WAO KWA MOLA WAO, WALA HAITAKUWA KHOFU JUU YAO WALA H WATA HUZUNIKA”
Ewe Mwenyezi Mungu , kila atakaye kunjua mkono wake na kutoa kwako basi mtengenezee mambo yake hapa Duniani na Kesho Akhera.
No comments:
Post a Comment