Saturday, March 24, 2012

NUFAIKA / FAIDIKA NA B.M.D.E ELIMU KWA NJIA YA MASWALI NA MAJIBU

.

NAITWA ISMAILI RAMADHANI
BOX 104 KINONDONI
DAR ES SALAAM.                                         
SWALI (A)     Mara nyingi nimekuwa nikiikosa swala ya jamaa kufuatana na kioksi changu, hivyo nimekuwa nikiswalia nyumbani kwangu, hivi swala zangu hapa napata thawabu au vipi?

SWALI(B)      Nilivyosoma mimi katika lugha ya kiarabu neno jamaa huanzia na watu au vitu vitatu, hivi tunaposema swala ya jamaa, inamaanisha inaanzia na mtu mmoja au watatu kama nilivyo soma mimi? naomba nifahamisheni.

JIBU(A)   Kwanza ifahamike vema kuwa swala ya jamaa ni fardhi kifaayat (nguzo) kama ilivyo swala jenaiza yameelezwa hayo katika vitabu vitu vya sheria na walimu wanatufunza jambo hilo kila siku, nalengo kuu ya swala ya jamaa nikuleta muungano kwa waislamu (unity) na kuondoa kabisa mtengano (veriety) nazimepokelewa hadidhi nyingi tu juu ya kuhimizwa swala ya jamaa, mimi nanza na hii :- amesema mtume mtukufu (saw) kwamba, laukama watu wangejua ubora naladhima zilizopo katika swala ya jamaa basi wangelileta hata kwa kutambaa (kama wangekuwa ni vilema) hapa mtume mtukufu (saw) anahimiza swala ya jamaa (hata kama mtu angekuwa kilema hana miguu)
FADHILA ZA SWALA YA JAMAA.
Amesema mtume mtukufu (saw) kwamba: swala ya  jamaa inaizidi fadhila swala ya mwenye kuswali pekeyake kwa madaraja ishirini na saba na katika mapokezi mengine katika hadidhi sahihi kabisa aliyoipokea imamu Bukhary kutoka kwa mtume mtukufu (saw) amesema swala ya mtu katika jamaa inaizidi swala yake yakuswalia nyumbani au sokoni kwake mara ishirini na tano (25) hii ni kwa ajili ya hatua anazotumia mtu huyo kwa ajili ya mola wake.

Hivyo shughuli zetu zisitutawaler mpaka tukaacha swala ya jamaa, tazama swahaba huyu aliyekuwa kipofu Abdallah bin ummimaktuum alivyokatazwa kuswalia nyumbani pamoja na tatizo lake la upofu. Hii ni pale alipo mjia mtume mtukufu (saw) kasha akamwambia hivi:-

Ewe mtume mimi nikipofu na usiku ni kiza njiani kuna mashimo, je unaweza kunipa ruksa ya kuswali nyumbani swala ya isha na alfajiri kufuatana na tatizo langu la upofu mtume alijibu hivi; sikupi ruksa hata kidogo kwa ajili ya ubora na umuhimu wa swala ya jamaa.

Tazama huyu ni kipofu amenyimwa amenyimwa ruksa ya kuswalia nyumbani je sisi wenye macho ingekuwa vipi?
Pia mtume mtukufu (saw) alipata kusema hivi:- namuapia muenyenzi mungu ambaye nafsi yangu imumikononi mwake, kwa hakika nimekusudia kuamrisha zikatwe kuni halafu uwashwe moto, kasha niwaamrisha watu kuswali kasha itolewe adhana ,kasha nimrishe mtu awaongeze watu, kasha nitoke niwaendee watu wanayo ikhalifu swala ya jamaa nikawaunguzie manyumba yao kwa kosa hilo ( lakuhacha jamaa) .
Hii hadidhi sahihi kabisa inayowahimiza watu waswali swala ya jamaa, wasiache pamoja na kuwa uwezo wa kuetekeleza. Hivyo fahamu kazi kuwa swali ya jamaa ni fardhi kifaayat kwa mtu mkazi isipokuwa kwa msafiri ni suna muakadat hata lazimika kuiswali.

JIBU (B)         Neno jamaa kisheria katika swala huanzia na watu wawili imamu na maamuna nakuendelea……….
Na kilugha huanzia na watu watatu au vitu vitatu na kuendelea……………
Naswalaa ya jamaa huwakusanya wanaume na wanawake pia.
            FAIDAT WAFURUU SHARIAT.
Mwanaume unapo swalia nyumbani anapata daraja moja na anapo swalia jamaa kama msikitini kama upo anapata daraja ishirini na saba.
Mwanamke anapo swalia nyumbani anapata daraja ishirini na saba na anapo swalia msikitini anapata daraja moja.
                                    Walaahu aalamu.


No comments:

Post a Comment