Wednesday, March 28, 2012

VIJANA WA LEO





Tukumbuke jamani leo hivi tunafanya ujeuri katika mgongo huu wa ardhi kwa vile ni mpana, kesho tutakapoingia katika tumbo la ardhi, hakika hatutakuwa na sehemu ya kukimbilia. Katika tumbo la ardhi ni matendo mema tu ndio yatakufanya uwe katika amani, kama hauna matendo mema basi misukosuko itakupata.

Kwa kweli vijana wa leo ni waajabu kabisa, yaani mtu anaweza kumuona mgonjwa wa UKIMWI, kusikia au kusoma kuhusu gojwa la UKIMWI, atafikiri na kujuta kwa muda ule, akitembea hatua moja kutoka sehemu ya tukio basi anasahau kila kitu. Vipi vijana tunashindwa kuzimiliki akili zetu na utashi wetu.
Leo viwanja vimejaa miba, miiba ambayo ikituchoma tutapata mateso ya kuumwa sana na kesho tutaadhibiwa na Mwenyenzi Mungu juu ya zinaa. Hakika leo hivi tujue fika alama za kiama zimekwisha dhihiri, kwa hiyo tufanye maandalizi ya kuiaga hii dunia. Maandalizi yenyewe ni kurejea kwa muumba wetu na kufuata hukumu zake.

Leo hivi vijana wa kiume wakiona sketi (msichana) inapita, utasikia minong’ono. Wengine watasema angalia mzigo, wengine watasema angalia bonge la mlima au kiuno angalia demu na sifa nyingine watazitoa. Vijana wakike nao wakimuona mvulana au suruali anapita utasikia wakisema cheki buzi, kifaa, kidume, meni na mengineyo, maneno haya yote yanaonesha jinsi gani vijana tulivyotawaliwa na ibilisi.

Vijana hivi leo tunapokutana katika jumuiya mbalimbali kama katika vyuo, sekondari, na mikusanyiko mingine tukawa jinsi tofauti  basi kila mmoja atakuwa na tamaa ya kuwa na mpenzi. Jambo hili ni hatari sana kwa maisha yetu, maisha ya hapa duniani na kesho Akhera.

Hatari hapa duniani kwa vile  huwa tunachanganya suala la masomo na mapenzi, mapenzi yanaweza kutupotezea muda, mapenzi yanaweza kutufanya tuwe maskini kwa vile ndani yamapenzi ni vitu vya gharama ndivyo hutawala. Sivyo hivyo tu bali suala la magonjwa yazinaa hasahasa huyu muuaji wa furaha (A killer of joy) UKIMWI.

Ndugu zangu  hakuna njia ya mkato ya kuepukana  na huyu muuaji wa furaha (A killer of joy) bali ni kurejea kwa mola wetu. Tukirejea kwa mola wetu hakika tutafanya yale aliyo tuamrisha na kuacha yale aliyoyakemea. Kwa kufanya hivyo ndio amani kwetu. Kwa hiyo tukiendeleza zinaa tutateseka duniani na kesho akhera tutateseka.

Vijana wezangu hebu tujiulize tunapokutana katika jumuiya mbalimbali na kuwa na tama ya kuwa na mpenzi. Je kila mmoja anamjua mwenzake , anajua alikotoka ana tabia gani, je anakuwa na uhakika gani kuwa yuko salama, je anakuwa anavunja amri ya mungu   ya sita, inatuonya tusizini? Je tunaipinga ile aya inayotukataza tusikaribie zinaa.KUMBUKA EWE NDUGU YANGU KUWA HAYA TULIYONAYO NDIO MAISHA YENYEWE, HAKUNA MAISHA MENGINE ZAIDI YA HAYA TULIYONAYO KWA MAISHA YA HAPA DUNIANI.






  

No comments:

Post a Comment