Wednesday, March 28, 2012

SHEITANIMTU NI NANI?



Sheitanimtu anaweza kuwa jamaa yako, ndugu yako, rafiki yako au wewe  mwenyewe. Sheitanimtu ni kila anayeweza kumpoteza mtu akatenda jambo ovu kama vile kuiba, kuzini, kunywa pombe, kuvuta bangi na kutumia madawa ya kulevya au kukupandikiza chuki baina yako na mwengine.

Sheitanimtu kila siku unatembea naye, unakula naye lakini huwezi kumgundua kwa urahisi wakati wote unapokuwa nae hujifanya anaushari, busara  na hekima upande wako kiasi kwamba wewe mwenyewe humpenda na kumwamini kwa kumuamini na kumthamini kwako basi anajenga katika akili yako mizizi ya tabia na mwenendo wake na hivyo kukufanya uwe miongoni mwa tawi lake.

Ewe ndugu yangu sheitanimtu hafanyi mambo yake kwa siri bali hufanya kwa uwazi ili wewe uyaone na uweze kushawishika. Anaweza kunywa pombe mbele yako kutumia madawa ya kulevya, kuvuta bangi na anaweza kukusimulia jambo lolote kama uzinzi n.k vitendo na masimulizi hayo yote ni kukuvuta wewe kutoka tabia nzuri kukupeleka katika tabia mbaya.

Rafiki yangu mpendwa huyo sheitanimtu yuko tayari kutumia hata gharama ilimradi tu akupoteze. Anaweza kununua vitu vya gharama ili akupe wewe akitaka uwe tu pamoja naye katika maovu. Hapa siyo kwa jinsi yako tu, msichana anaweza kugharamiwa na mvulana au mvulana anaweza kugharamiwa na msichana kwa ajili ya kufanya uovu. Jambo hili ewe ndugu yangu ni hatari sana kwani wewe unajua fedha ni fedheha.

 Ewe ndugu yangu, wewe unaakili timamu na unajua ukweli wa mambo unajua yenye manufaa na hasara katika maisha ya kila siku. Kutokana na akili uliyokuwa nayo huna budi kuwa makini na kutafakari wakati unapopewa ushauri na huyo ambaye unasema rafiki yako. Tafadhali sana usipende kusema “ndiyo” au “hapana” bila kufikiria faida au madhara ya hiyo  NDIO AU HAPANA  yako.

Bila shaka wewe unapenda kuisha kwa amani na furaha karibu kila siku kwa hiyo huna budi  kuwa makini katika ,maisha yako. Umakini ambao ninakuambia ni “KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA” suala hili la kufikiri kabla ya kutenda litakufanya uweze kugundua mbinu na ujanja anaotumia huyo sheitanimtu na hivyo kujiepusha naye mimi sipendi kuona wewe rafiki yangu  ukiwa katika huzuni na majuto ndio maana nina kupa mwanga katika maisha yako.

Ndugu yangu, sheitanimtu katika maisha yako ujitahidi kamuogopa kama ukoma jiepushe nae na asikuzoe nakukutawala katika akili yako na kukufanya wewe kuwa mtu usiyekuwa na kauli ya kusema HAPANA katika kila jambo la uovu.

Wewe ni rafiki na ni ndugu yangu, ninakupa mwanga huu kwa manufaa yako mwenyewe na sio kwa manufaa yangu. Nijukumu lako kutumia akili na hekima alizo kupa Mungu ili uweze kuepukana na sheitanimtu, nawe utaifanya akili yako ifanye kazi kama inavyo  takiwa. Kama ulikwisha potenzwa siyo ukate tamaa bali tumia  muda huu kujuta na kujirekebisha mara moja.

                        UJUMBE HUU UMETOLEWA NA
                        MWL: NAHONYO (FAKIHI SALUMU MSHAMU)
                                   
           







No comments:

Post a Comment