Wednesday, March 28, 2012

VIJANA WA LEO




  Ewe kijana mwenzangu mbona unajisahau na kuzama katika dunia hii na kusahau kesho Akhera (mbinguni)? Ewe rafiki yangu mbona unazidi kumsahau mungu wako na kuzama katika mac hafu yanayo mc hukiza muumba wako eti unasema “ we go up to date (tunaenda  na wakati)” Jamani ni kweli kwenda na wakati ni kufanya matendo machafu? Unaonaje ukienda na wakati hali ya kuwa unafanya yale yaliyokuwa  mazuri yaku mfurahisha muumba?

Kijana mwezangu wakati wa ujana ndio wakati wa mitihani mingi nandio wakati wa matamanio mengi. Vijana wa leo kukicha tunaipamba miiliyetu na dunia hii kwa kwa  machafu kabisa tuna sahau kufanya vitando vizuri ambavyo vitatupatia mafanikio katika maisha yetu ya hapa duniani na kesho akhera (mbinguni). Kutokana na kuji sahau kwetu wengi miungoni mwetu tunabaki katika kilio na majuto kutokana na tabia na mienendo yetu.

Mwenyenzi mungu ametuumba wanadamu akatupa uwezo kuliko viumbe wengine. Akatupa elimu, akatupa uhuru wa kuweza kupanga na kupangua, kusuka na kufumua, kupanda na kushuka, kucheka na kulia, kuzama na kuibuka, kufunga na kufungua na mengine mengi. Pia mwenzi mungu ametujalia akili ambayo inatusaidia kupambanua mambo mbali katika maisha yetu ya kila siku.

Pamoja na mwenzi mungu kutujalia akili, pia ametujalia macho, mikono, miguu, mdomo nahivyop vingine. Basi tunapo tumia akili zetu vibaya , macho yetu kuyatumia kwa kutazama yale yaliyo haramishwa, midomo yetu tukaitumia vibaya  kama vile kutukana, kusengenya na kugonganisha watu, masikio yetu tuka yatumia kusikiliza mabo ya kipuuzi, mikono yetu tukaitumia kwa kunyang’anya na kupiga watu na miguu yetu tukaitumia kamachombo cha usafiri wa kuyaendea yale yaliyo katazwa basi tujue kuwa tutakuwa miongoni mwa watu wenye khasara.

Vijana wa leo tunavaa mavazi kinyume na tunavyo takiwa kuvaa yaani wanaume wanavaa mapambo ya kike na wanawake wanavaa nguo za kiume. Siyo hivyo tu bali mavazi yenywe hayana sifa. Kwa mfano zina kuwa fupi, zenye kubana na zinazoonesha sehemu ya ndani ya mwili (transparent).

Jambo jengine vijana wezangu ni kuhusu vijana wa kiafrika (weusi) kujibadili rangi, yaani tunaukataa uafrika (self alienation). Jamani mwenye mungu ameumba mwanadamu kwa umbo lililobora kabisa, sasa vipi tuna kataa weusi? Mbona wezetu hawajipaki masinzi iliwawe weusi kama sisi? Unafikiri wao hawaitaki rangi yetu, wao wanatami rangi yetu nyeusi lakini wanakubali na kuridhika na rangia aliyo wapa mwenyenzi mungu. Jamani kwa nini sisi tunajidharau nakutaka kuiga rangi zao?
Vijana wa kike mwenyenzi mungu amewapa nywele nzuri kabisa (nyeusi) lakini wala hawaridhiki, matokeo yake wanaamua kuweka nywele zao dawa na wengine wanaweka nywele za bandia (maiti). Lazima tuelewe kuwa kufanya hivyo tunamkashifu muumba wetu yaani tunamuona hawezi kuumba, bora tujifinyange wenyewe. Kutokana na tamaa zetu wengine wanabaki na majuto, kwa mfano hebu muangalie huyo rafiki yako jinsi alivyo utazani anaumwa kansa ya ngozi vile.
Enyi vijana wezangu tujiulize, hivi wanaume wakivaa mavazi mazuri tena ya heshima, wakaacha kuvaa mapambo ya kike kama vile heni, mikufu bangili na mengineyo na wakaacha ,kunyoa mitindo ya ajabu, hawawezi kupendeza? Kama wanaweza kupeza na kupendwa kunaumuhimu ,kuongeza mambo mengine ya karaha?
Naona vijana wa kike wakiacha kuvaa nguo za kiume.kujibadili rangi, kuvaa nguo fupi, kuweka nywele za maiti (bandia), hawawezi kupendeza ? hawawezi kupendwa? Kama watapendeza na kupendwa, je hayo mengine yana umuhimu gani?
Jamani mwanamume kuvaa mapambo ya kike kunyoa mitindo ya ajabu na kuvaa suruali za kubana wala sio dawa ya kupendeza na kupendwa, halikadhalika wanaume kuvaa nguo za kiume, kujibadili rangi, kuweka nywele za maiti (bandia) kuvaa nguo fupi na za kubana wala sio dawa ya kupendeza na kupendwa. Bali hayo yote ni kichocheo cha maovu.

Vijana wezangu mapamboa na mavazi yetu ni kero katika dunia yetu na ndio ufunguo wa zinaa. Mavazi ya kike zaidi ndio yanayo chochea dhinaa, kwani mwanamke anapovaa nguo zinazoonesha sehemu fulani huwa ni tattizo kwa wanamme, kwani kimaumbile mwanamume anaweza kushindwa kujizuiya kutokana na matamanio aliyoyapata kwa kuona sehemu fulani tu ya wawili na mwanamke. Tafadhali tumia fikra  zako na hizi ninazokupa ili ujirekebishe.



No comments:

Post a Comment